KISWAHILI SARUFI OLEVEL

      SARUFI
Sarufi nimfumo na kanuni za lugha zinazomwezesha mtumiaji wa lugha kuitumia lugha husika kwa usahihi. Mfumo huo humwezesha mzungumzaji kutunga sentensi zisizo na kikomo ambazo hukubalika na wazawa wa lugha wanaoifahamu lugha hiyo barabara.  Hivyo ni dhahiri kwamba kila lugha ya mwanadamu huwa na mpangilio na sheria zinazoilinda ili kuifanya kuwa toshelevu na sanifu, na uzingatiwaji wa kanuni na taratibu hizo kwa mtumiaji humfanya na kumtambulisha kama mmilisi wa lugha hiyo.
Sheria za lugha zimegawanyika katika makundi manne yanayojulikana kamamatawi ya Sarufi ambayo ni pamoja na; matamshi, maumbo, muundo na maana.

1.      SARUFI MATAMSHI
Sarufi matamshi ni tawi la sarufi ambalo limejikita katika kuchunguza sauti na matamshiyanayotumika katika lugha Fulani na kulinda matumizi sahihi ya matamshi hayo baina ya watumiaji wa lugha hiyo. Lugha ya Kiswahili kama zilivyokuwa lugha zote duniani ina matamshi ya aina mbili; Irabu na konsonanti.
A.    Irabu
Irabu ni aina ya vitamkwa ambavyo hutolewa pasi na kuwepo kizuizichochote katika mkondo hewa utokao mapafuni ukipitia katika chemba ya kinywana chemba ya pua kwenda nje. Lugha ya Kiswahili inazo Irabu tano ambazo ni; /a/, /e/, /i/, /o/, na /u/.
B.     Konsonanti
Konsonanti ni aina ya sauti ambazo hutamkwa kwa kuzuia mkondo hewa kutoka mapafuni, ukipitia chemba ya kinywa na chemba ya pua kwenda nje. Katika lugha ya Kiswahili zipo jumla ya konsonanti zifuatazo; /b/, /ch/, /d/, /dh/, /f/, /g/, /gh/, /h/, /j/, /k/, /l/, /m/, /n/, /ny/, /ng’/, /p/, /r/, /s/, /sh/, /t/, /th/, /v/, /w/, /y/ na /z/.



2.      SARUFI MAUMBO.
Hili ni tawi la sarufi ambalo hujishughulisha na uchunguzi wa maumbo mbalimbali ya maneno katika lugha ya Kiswahili. Maumbo hayo ni; silabi, mofimu na neno lenyewe.

A.    Silabi
Silabi ni kipashio cha kifonolojia kinachohusu matamshi ambacho kwacho sauti za
Lugha hutamkwa mara moja kwa pamoja kama fungu moja la sauti. Kuna aina mbili za silabi, yaani silabi fungenasilabi huru.
Silabi huruni zile ambazo huishia na irabu.
Kwa mfano; la, ma, kwa, mba, n.k.
 Ilhalisilabi fungeni zile zinazoishia na konsonanti ambapo katika lugha ya Kiswahili ni nadra kuzipata maana lugha hii inatumia silabi huru lakini hupatikana katika maneno ya Kiswahili yanayokopwa kutoka katika lugha nyingine.
            Kwa mfano;   Alhamisi – a-l-ha-mi-si
                                    Taksi     - ta-k-si
Miundo ya Silabi za Kiswahili
a.      Muundo wa irabu peke yake (I) - Yapo maneno katika lugha ya Kiswahili yanayoundwa na irabu peke yake kama silabi. Mfano; u+a = Ua, o+a = Oa, a+u = Au, n.k.
b.      Muundo wakonsonanti pekee (K) – Kiswahili hakina maneno mengi yanayoundwa na silabi pekee isipokuwa maneno machache ambayo huwa ni ya nazali /M/ na /N/ na huwa zinatumika ama mwanzoni au katikati ya neno. Mfano; m+ke = Mke, m+bwa = Mbwa, n+chi = Nchi n.k
c.       Muundo wa konsonanti na irabu (KI) – Katika muundo huu konsonanti hutangulia irabu. Mfano; b+a = Ba, k+a = Ka n.k.
d.      Muundo wa konsonanti mbili na irabu (KKI) – Katika muundo huukonsonanti mbili hutangulia irabu. Mara nyingi konsonanti ya pili huwa ni kiyeyusho. Mfano; k+w+a = Kwa, m+w+a = Mwa, b+w+a = bwa, n+d+e = Nde, n.k.
e.       Muundo wa konsonanti tatu na irabu (KKKI) – Muundo wa namna hii hujitokeza katika maneno machache. Mfano; Bambwa, Tingwa, Tindwa, Mbwa, n.k.
f.       Muundo wa silabi funge – Huu hujitokeza katika maneno machache ambayo huwa ya mkopo. Mfano; Il-ha-li = Ilhali, Lab-da = Labda
B.     Mofimu
Mofimu ni kipashio kidogo kabisa cha lugha ambacho kina uwezo wa kusitiri maana ya neno ambalo kwalo limeundwa. AU ni kipashio kidogo kabisa cha lugha chenye maana kisarufi.

                                    AINA ZA MOFIMU
Mofimu huru ni aina ya mofimu ambayo huweza kusimama pekee na kujitosheleza kimaana yaani huwa na sifa ya neno. Mfano; mama, Baba, Dada, Kaka, Mjomba, Shangazi n.k. Kwa kuangalia utagundua kuwa mofimu huru haziwezi kugawanyika zaidi na kubeba maana kisarufi, kwa maana kwamba mofimu ‘baba’ ikigawanywa ba-ba, ‘ba’ hii haina maana yoyote kisarufi zaidi ya kuwa silabi.

Mofimu tegemezini aina ya mofimu ambayo huweza kuvunjwavunjwa na kubeba maana kisarufi, mofimu tegemezi hutegemeana ili kuleta maana kamili ya neno.
Mfano; neno ‘anakula’ limeundwa na mofimu zifuatazo:- [a-na-kul-a] ambazo kila moja hubeba dhana Fulani ya kisarufi.

VIAMBISHI
            Ni mofimu zinazopachikwa nyuma au mbele ya mzizi wa neno ili kubadilisha dhana ya neno. Kwa kuwa mofimu hizo hupachikwa sehemu mbili tofauti, tunapata aina mbili za viambishi kwa mujibu wa nafasi zake katika nenoyaani; viambishi awaliambavyo hupachikwa mwanzoni au nyuma ya mzizi wa neno,viambishi katiambavyo hupachikwa katikati ya neno (Kiswahili hakina viambishi hivi) na viambishi tamatiambavyo hivi hupachikwa mbele au mwishoni mwa mzizi wa neno.
Mfano:-
VIAMBISHI AWALI
MZIZI WA NENO
VIAMBISHI TAMATI
NENO JIPYA
    A
    na
           chez
     ew
    a
Anachezewa
    Wa
     li
           chez
     ean
    a
Walichezeana
    Tu
    ta
           chez
     e
    a
Tutachezea


1.      Viambishi awaliHivi hupachikwa kabla ya mzizi wa neno na huwa ni vya aina tisa:-
i.                    Viambisha awali vya nafsi- hivi hudokeza upatanishi wa  nafsi katika kitenzi, zipo nafsi tatu, nafsi ya kwanza, ya pili, nay a tatu.

NAFSI
UMOJA
UWINGI
Ya Kwanza
Ni-
Tu-
Ya Pili
U-
M-
Ya Tatu
A-
Wa-



M


Mfano:-Ninalima
            Tunacheza

ii.                  Viambishi awali vya ngeli- hivi hupatikana mwanzoni mwa nomino au vivumishi ili kudokeza hali ya umoja na uwingi.

Mfano:-Mtu (umoja) – Watu (uwingi)
            Msafi (umoja) – Wasafi (uwingi)

iii.                Viambishi awali vya ukanushi - hivi hudokeza hali ya uhasi wa tendo. Huwakilishwa na mofimu (ha-) na (si-)

Mfano:- Amekula (uyakinifu) – Hajala (ukanushi), Nakula (uyakinifu) – Sili (ukanushi)
iv.                Viambishi awali vya Njeo- hivi hudokeza nyakati mbalimbali ambazo ni wakati uliopita, uliopo na ujao.

NYAKATI
MOFIMU
Uliopo
-Na-
Uliopita
-li-
Ujao
-Ta-

            Mfano:- Mlituona
                          Utakuja

v.                  Viambishi awali vya hali- hivi hudokeza hali mbili za nyakati ambazo ni mazoea ambayo huwakilishwa na mofimu {hu} na timilifu inayowakilishwa na mofimu {me}.
Mfano:-Hucheza
              Amelima

vi.                Viambishi awali vya masharti-hivi hudokeza hali ya masharti au uwezekano katika tendo. Mofimu hizo ni kama –ki-, nge-, ngali- n.k.

Mfano:- ukija
              Ungekuja
               Angalimkuta

vii.              Kiambishi cha urejeshi wa mtenda (kiima)- mhiki hudokeza urejeshi wa nomino inayotenda katika kitenzi.

Mfano: - Aliyekuja {-ye-} hudokeza urejeshi wa mtenda.

viii.            Kiambishi kiwakilishi cha mtendwa au mtendewa (shamirisho) – hivi huwakilisha mtendwa au mtendewa wa jambo.
Mfano; Nilimpiga, Uliukata, Nimeipenda, Wameniteta.

ix.                Kiambishi awali cha kujirejea (kujitendea) – hiki huwakilishwa na mofimu (-ji-)
Mfano; kujipenda

2.      Viambishi tamati– Hivi hudokeza kauli mbalimbali za vitenzi.
Mfano: - Anacheza – kutenda
Unachezwa- Kutendwa
              Utachezewa- Kutendewa
               Nimemlia- Kutendea
              Wamewasomesha- Kutendesha n.k

Mzizi
Kiambishi cha Kauli
Kiambishi tamati maana
Neno jipya
Kauli
Viambishi vya kauli
Chez

a
Cheza
Kutenda
-a

e
a
Chezea
kutendea
-e-
Pig
ian
a
Pigiana
Kutendeana
-ian-/-ean-

iw
a
Pigiwa
Kutendewa
-iw-/ew-
Som
esh
a
Somesha
Kutendesha
-ish-/esh-

eshw
a
Someshwa
Kutendeshwa
-ishw-/eshw-
Lim
ik
a
Limika
Kutendeka
-ik-/-ek-

an
a
Limana
Kutendana
-an-

w
a
Limwa
Kutendwa
-w-

DHANA YA MZIZI NA SHINA LA KITENZI

Mzizi wakitenzini sehemu ya neno inayobakia mara baada ya kuondoa viambishi vyote vya awali na tamati katika neno hilo. Mfano: - a-na-chez-a {-chez-}, m-ku-lim-a {-lim-}
Mzizi fungeni ule ambao hauwezi kujikamilisha kimaana yaani hauwezi kusimama kama neno. Mfano; -lim-, -chez-, -imb- n.k.
Mzizi huruni ule ambao huweza kusimama kama neno na ukichanganuliwa zaidi hupoteza maana yake ya msingi. Mfano; Kinu, Kazi, Arifu, Sali n.k.


Shina la kitenzini sehemu ya neno ambayo huongezwa viambishi fuatishi (tamati) au nisehemu ya neno ambayo hubakia baada ya kuondolewa viambishi tangulizi. Mfano:- chez+a = cheza, lim+a = lima. Sehemu hii ya neno hutumika kuundia neno jipya.
Shina sahili – hili ni shina ambalo huundwa na mofimu moja tu ambayo ni mzizi wa neno hilo, huwa ni mofimu huru, Mfano; Kesho, jana, kitabu, jarida n.k.
Shina changamano – shina hili huundwa na mzizi na kiambishi tamati maana. Mfano; cheka, lala, lia, kula n.k
Shina ambatani – shina hili huundwa na mofimu mbili ambazo ni huru. Mfano; mwana + kwenda = mwanakwenda, mbwa + mwitu = mbwamwitu

           
UAMBISHAJI NA MNYUMBULIKO WA MANENO
Uambishaji
Uambishaji ni ule utaratibu wa kuongeza viambishi katika mzizi wa neno, ili kulipa neno maana ya ziada. AU ni hali ya kubadilishabadilisha mofimu katika mzizi wa neno ili kuonesha upatanisho wa kisarufi katika tungo hiyo.
Kiambishi:
Kiambishi ni sehemu (mofu) ambayo huambikwa kwenye mzizi wa neno ili kulipa neno hilo maana ya ziada. Tunapopachika viambishi hivyo mwanzoni mwa mzizi wa neno hali hiyo huitwa ‘uambishaji’. Uambishaji upo wa aina mbili; Unyambuaji au unyambulishi: Huu ni aina ya uambishaji unaosababisha neno kubadilika kutoka kategoria moja hadi nyingine. NaMnyambuliko:Ni aina ya uambishaji ambao huhusisha kurefusha nenona kuliweka katika hali tofauti za katagoria ileile.
Uambishaji wa kategoria mbalimbali za maneno.
Uambishaji wa vitenzi – Uambishaji wa vitenzi hujitokeza kwa kutegemea dhima tofauti tofauti za mofimu kama vile:-
        i.            Viambishi vya nafsi
      ii.            Viambishi vya njeo
    iii.            Viambishi vya ukanushi
    iv.            Viambishi vya urejeshi
      v.            Viambishi vya hali
    vi.            Na viambishi vya kujitendea
Mfano; mzizi –lim- unaweza kupachikwa viambishi hivyo na kuweza kubadilika kidhana kama ifuatavyo:-
A-na-lim-a
Hu-lim-a
U-me-lim-a
Ni-na-vyo-lim-a n.k.

Uambishaji wa majina– Uambishaji wa majina huwa unazingatia upatanisho wa kisarufi kimofolojia ambao hujikita katika kuangalia alomofu tofauti zinazowakilisha ngeli moja katika umoja na uwingi wa majina hayo.  Kwa mfano:-
UMOJA
WINGI
ALOMOFU
m-tu
Wa-tu
M/WA
m-ti
mi-ti
M/MI
Ki-ti
vi-ti
KI/VI
u-gonjwa
Ma-gonjwa
U/MA
Ø-fisadi
Ma-fisadi
Ø/MA
Ø-kaka
Ø-kaka
Ø/ Ø

Uambishaji wa vielezi– Vielezi katika lugha ya Kiswahili havitokani na kategoria nyingine ya maneno, bali ni maneno ya kawaida yanayopatikana katika lugha na si rahisi kupachika mofimu yoyote katika maneno hayo isipokuwa vielezi vichache ambavyo hupatikana kwa kupachikwa kiambishi awali cha namna {ki-} katika kivumishi au nomino mfano: ki-jinga, ki-janja, ki-toto, ki-raia, ki-puuzi n.k.
Unyambulishaji
Ni hali ya kupachika viambishi tamati katika mzizi wa neno. Mofimu hizo huitwa mofimu fuatishi.
Unyambulishaji wa kategoria mbalimbali za maneno ya Kiswahili.
        i.            Viwakilishi. Mfano; Mimi = miye, Sisi = siye, Ambalo, Ambacho, Ambao, Ambaye n.k.
      ii.            Majina. Mfano: Nyumba+ni = Nyumbani, Shamba+ni = Shambani, n.k.
    iii.            Vivumishi. Mfano: Safi = Safisha, Refu = Refushan.k.
    iv.            Vitenzi. Mfano: Lima-limika-limishwa-limwa-limiana-limiwa n.k.
Ukitazama kwa makini utangundua kwamba unyambulishaji mara nyingi hubadilisha neno kutoka katika kategoria moja na kuipeleka katika kategoria nyingine.
DHIMA ZA UNYAMBULISHAJI
        i.            Kuongeza msamiati wa lugha ya Kiswahili.
      ii.            Kuzalisha kauli mbalimbali za vitenzi vya Kiswahili
    iii.            Hupanua maana ya neno.




TABIA ZA VITENZI VYA KISWAHILI
            Vitenzi vya Kiswahili huwa na tabia tofauti tofauti zinazotokana na dhima za mofimu ambazo hupachikwa katika vitenzi hivyo, hivyo kulingana na dhima za mofimu, vitenzi vya Kiswahili huwa na tabia zifuatazo:-
       I.            Kutambulisha nafsi. Mfano:- Anayesoma
    II.            Kutambulisha tendo. Mfano:- Cheza, Lima, Imba n.k.
 III.            Kutambulisha wakati. Mfano:- Ulikuja
 IV.            Kutambulisha hali ya uyakinishi na ukanushi. Mfano:- Anacheka – Hacheki
    V.            Kutambulisha kauli mbalimbali za tendo. Mfano:- cheza-chezwa-chezewa-chezeka n.k.
 VI.            Kutambulisha hali ya tendo. Mfano:-Huimba, Amekula.
VII.            Kuonesha urejeshi wa mtenda, mtendwa na mtendewa ambao hujidhihirisha katika ngeli ya nomino iliyotajwa kwa kuzingatia upatanisho wa kisarufi. Urejeshi huo ni wa O-rejeshi. Katika urejeshi huo vitenzi hubeba viambishi ngeli vya –O- isipokuwa kama nomino ni ya ngeli ya kwanza umoja  ambapo hutumia –e- badala ya –O-.
Mfano:-
NGELI
KIAMBISHI CHA O- REJESHI
MFANO
A-WA
-YE- na –O-
Aliyepiga / Waliokuja
U-I
-O- na –YO-
Uliokatwa / Iliyokatwa
LI-YA
-LO- na –YO-
Lililochanika / Yaliyochanika
KI-VI
-CHO- na –VYO-
Kilichovunjika / Vilivyovunjika
I-ZI
-YO- na –ZO-
Iliyofungwa / Zilizofungwa
U-ZI
-O- na -ZO
Uliokatika / Zilizokatika
U-YA
-O- na –ZO-
Ulionipata / Yaliyonipata
KU
-KO-
Kulikotokea
PA-MU-KU
PO-MO-KO
Pale alipoingia / Mule alimotokea / Kule alikofunga




ZOEZI
1.      Fafanua dhana ya sarufi kisha eleza tanzu zinazoijenga.
2.      Eleza umuhimu wa kujifunza sarufi ya Kiswahili.
3.      Onesha tofauti iliyopo kati ya irabu na konsonanti.
4.      Eleza maana ya silabi na uoneshe kwa mifano miundo mitano ya Silabi za Kiswahili.
5.      Nini maana ya mofimu? Fafanua aina zake.
6.      Bainisha dhima za kila mofimu katika maneno yafuatayo:-
a.       Anakula
b.      Waliokutafuta
c.       Tulipokukosa
d.      Nikikukumbuka
e.       Aliyempigia
f.       Hakufika
g.      Huimba
h.      Mnavyopendana
i.        Amemtukana
j.        Ungelifika
7.      Nini maana ya uambishaji na mnyumbulkiko wa maneno? Onesha jinsi dhana hizo zinavyochangia kukuza lugha.
8.      Eleza kauli mbalimbali za vitenzi vya lugha ya Kiswahili.
9.      Pachika viambishi ngeli vya O- rejeshi katika vitenzi vifuatavyo ukibainisha umoja na uwingi:-
a.       Chura amekufa
b.      Kitabu kimechanika
c.       Meza imevunjika
d.      Daftari limechanika
e.       Simu imeita
f.       Ameingia mahali humu
g.      Amepitia pale
h.      Imevunjiwa kule


10.   
C.     Neno
Ni silabi au mkusanyiko wa silabi zinazotamkwa au kuandikwa ambazo huwa na maana (maana yaweza kuwa ni ya kileksika au kisarufi).

AINA ZA MANENO

1.      NOMINO
Ni aina ya neno ambalo hutaja mtu, kitu, mahali, hali na kitendo. Mfano; Mwajuma, Kalamu, Mwanza, Udakitari, Kulima n.k.

Aina za nomino:
·         Nomino za pekee: Nomino za pekee hutaja na kutambulisha nomino mahsusi
na za kipekee. Yaani kuwa kitu ni hicho na wala si chengine chochote. Hizi ni nomino zinazohusisha majina kama vile ya watu, nchi, miji, mito, milima,maziwa na bahari. Herufi za kwanza za nomono za pekee huwa kubwa hata kamanomino hizi zinapatikana katikati ya sentensi. Mfano; baba, Asha, Tanzania, Dodoma, Kilimanjaro, Victoria n.k

·         Nomino za jamii: Hizi kwa jina jengine huitwa nomino za jumla. Nomino hizihazibainishi wazi wazi vitu ambavyo habari zake zinatolewa. Kwa mfano ikiwa nimtu, mahsusi hatambuliwi. Haituambii kama ni Kelvin, Tuafu ama Zawadi.Ikiwani ziwa halitambuliwi kama ni Michigan , Victoria au Nyasa, yaani hutaja vitubila kutaja umahsusi wake kama ilivyo katika nomino za pekee. Hizizinapoandikwa si lazima zianze kwa herufi kubwa isipokuwa zimetumiwamwanzoni mwa sentensi au zimetumika kama anuani ya kutajia kitu kama vileMkuu wa Sheria. Katika mfano huu ‘sheria’ kwa kawaida ni nomino ya kawaida,lakini hapa inaanza kwa herufi kubwa kwani inataja anuwani ya kipekee. Mfano wa nomino za kawaida ni; Mwanafunzi, Mwalimu, Mnyama, Mtazamaji, Askari n.k

·         Nomino za kawaida: Kundi hili la nomino hutumia kigezo cha uwezekano wakuhesabika kuziainisha. Hapa tunatofautisha kati ya nomino zinazowakilisha vitu vinavyohesabika kwa upande mmoja, na vile visivyohesabika kwa upande mwengine. Nomino ya vitu vinavyohesabika vitanda, nyumba, vikombe vitabu kadahlika. Zile zisizohesabika hurejelea vitu ambavyo hutokea kwa wingi na haviwezi kugawika, kwa mfano maji, mate, makamasi, maziwa, moshi, mafuta. Aghlabu nomino hizo huwa sawa katika umoja na wingi.

·         Nomino za kitenzi jina: Hizi ni nomino zinazohusu vitenzi . Huundwa kwa kuongezwa kiambishi {ku-} cha unominishaji kwenye mzizi wa kitenzi cha kitendo halisi ili kukifanya kiwe nomino. Mfano; Kulima, Kucheza, Kuimba n.k

·         Nomino dhahania: Hizi ni nomino ambazo hurejelea vitu vinavyoweza kuhusika na mwanaadamu kupitia milango ya hisia kama macho, mapua, masikio vidole na ulimi- yaani vitu ambavyo haviwezi kushikika, kuonekana, na kuonjeka. Mfano; Vita, Njaa, Ugonjwa, Shetani, Mungu n.k

2. Vivumishi
·         Ni maneno ambayohutoa ufafanuzi au maelezo ya ziada kuhusu jina ili kuitambulisha vyema.
Aina za vivumishi.
·         Vivumishi vya sifa: hutoa sifa za nomino /kiwakilishi cha nomino. Sifa hizi huweza kuwa nzuri, mbaya au yoyote ile.Mfano; mzuri, mbaya, mrembo n.k
·         Vivumishi vya idadi: vinaweza kujitokeza katika aina tatu ndogondogo.Vivumishivya aina hii hutoa taarifa kuhusu idadi ya nomino ambazo kiwango chakekimetajwa. Mfano; wawili, watano, wengi, wachache n.k
·         Vivumishi vya kumiliki: Ni vivumishi vinavyoonesha kuwa kitu fulani kina milikiwa na mtu au kitu chengine. Mfano;yangu, yake, yako, kwetu n.k
·         Vivumishi Vioneshi:Vivumishi vya aina hii huonyesha mahali au upande kitu kilipo. Vivumishi vya aina hiihujengwa na mzizi {h} kwa vitu vilivyopo karibu na mzizi {le} kwa vitu vilivyo mbali. Mfano; hapa, pale n.k
·         Vivumishi vya kuuliza: Hivi ni vivumishi ambavyo hufafanua nomino kwa kuuliza habari zake. Hujibu swali“gani?ipi? ngapi?”
·         Vivumishi vya pekee:Vivumishi hivi huitwa vya pekee kwa sababu kila kimojawapo huwa na maana maalumu.Pia kila kimojawapo huchukua upatanisho wake wa kisarufi kulingana na ngeli yanomino ambayo kinaivumisha. Mizizi vivumishi hivi niote, o-ote, enye, -enyewe, -ingine, -ingineo. –ote. Huonyesha ujumla wa kitu au vitu-o-oteKivumishi cha aina hii kina maana ya “kila”, “bila kubagua”– enyeKivumishi cha aina hii hutumika kuleta dhanna ya umilikishaji nomino Fulani. –enyeweKivumishi cha aina hii hutumika kuisisitiza nomino fulani.– ingineKivumishi cha aina hii huonyesha/huonesha ‘tofauti na’ au ‘zaidi ya’ kitu Fulani. – ingineoKivumishi cha aina hii hutumika kuonesha/kuonyesha ziadi.
·         Vivumishi vya A- unganifu: Vivumishi vya aina hii huundwa kwa mzizi wa kihusishi a- unganifu. Kihusishi hikihuandamana na nomino kuunda kirai husishi ambacho huvumisha nomino iliyotajwaawali. Vivumishi vya aina hii hutumika kuleta dhanna zifuatazo:--Umilikaji-Nafasi katika orodha. Mfano; wa kwangu, wa Juma, ya tano ya Sita n.k

4. Vielezi
Maana ya vielezi: Vielezi ni maneno yanayofafanua vitenzi, vivumishi auvielezi vyengine. Huweza kuarifu kitendo kilichotendeka kilitendeka wapi , namnagani na hata mara ngapi?

Aina za vielezi
·         Vielezi vya namna au jinsi.Vielezi vya namna hii huonyesha jinsi au namna kitendo kilivyotendeka. Vielezi vyanamna vipo vya aina kadhaa.
- Vielezi vya namna halisi.
Hivi ni vielezi vinavyotumia maneno ambayo kimsingi yana sura ya vielezi moja kwa
moja katika uainishaji wa aina za maneno.Mfano; kuimba sana
-Vielezi vya namna mfanano
Hivi ni vieleziambavyo hutumika kufananisha vitendo na vivumishi au nomino
mbalimbali. Hujengwa kwa kuongeza kiambishi (ki-) au kiambishi (vi-). Viambishi hivi
hujulikana kwa jina la viambishi vya mfanano.Ulifanya vizuri kumsaidia mwanangu.


-Vielezi vya namna vikariri
Hivi nivieleziambavyo hufafanua vitenzi kwa kurudiarudia neno moja mara mbili.Mfano; polepole, harakaharaka.
- Vielezi vya namna hali
Hivi nivieleziambavyo hufafanua juu ya kitendo kilichotendeka kimetendeka katika
hali gani. Mfano; kivivu, kibabe, kizembe, kipole n.k
- Vielezi vya namna ala/kitumizi
Hivi nivielezi vinavyotaja vitu ambavyo hutumika kutendea kitendo. Mfano; kwa kisu, kwa kalamu n.k
- Vielezi vya namna viigizi.
Hivi vinaelezea zaidi jinsi tendo lilivyofanyika kwa kuigiza au kufuatisha sauti
inayojitokeza wakati tendo linapofanyika au kutokea. Mfano; alimpiga paaaah!
·         Vielezi vya idadi. Vielezi vya namna hii huonyesha kuwa kitendo kilitendeka mara fulani au kwa kiasifulani. Mfano; amempiga mara mbili
·         Vielezi vya mahali..Vielezi vya namna hii huonyesha mahali ambapo kitendo kinatokea.Huweza kudokezwakwa viambishi au kwa maneno kamili. Mfano; amekaa jikoni
·         Vielezi vya wakati:Vielezi vya namna hii huonyesha wakati wa kutendeka kwa kitendo.Huweza kutokeakama maneno kamili au hodokezwa kwa kiambishi {po.}Mfano; alimkaribisha alipokuja.

5. VITENZI
Kitenzi ni neno linaloeleza jambo lililotendwa au lililotendeka. Kitenzi huarifu lililofanyika au lililofanywa na kiumbe hai chochote kinachoweza kutenda jambo. Kitenzi cha Kiswahili huundwa na mzizi pamoja na viambishi vyenye uamilifu wa aina tofauti.

                                    AINA ZA VITENZI
·         Vitenzi vikuu (T): Vitenzi vikuu ni vile ambavyo hubeba ujumbemuhimu wa kiarifu cha sentensi. Mfano; Mtoto amekuja.

·         Vitenzi visaidizi: Hivi hutoa taarifa ya kusaidia vitenzi vikuu. Hutoa taarifa kama vile uwezekano , wakati, hali n.k.Vitenzi visaidizi daima hutumika na vitenzi vikuu, ndivyo vinavyobeba viambishi vya wakati. Mfano; Alikua anacheza, Huwa namfurahia.
§  Vitenzi visaidizi huweza kupachikwa urejeshi wa nomino na kusaidia kuifafanua nomino hiyo. Mfano; motto aliyekua anacheza. Virejeshi hivyo ni kama; -ye-, -yo-,    -o-, -lo-, -cho-, -wo- n.k

·         Vitenzi vishirikishi: Hivi ni Vitenzi ambavyo hufanya kazi ya kuunga sehemu mbili za sentensi. Havichukui viambishi vya nafsi, njeo ama hali.Vitenzi vishirikishi ni vya aina mbili, ambavyo nikitenzi kishirikishi “ni” cha uyakinishi na kitenzi shirikishi“si” cha ukanushi.
Kazi za kitenzi kishirikishi
-kushirikisha vipashio vingine katika sentensi
-Kuonesha tabia fulani iliyopo au isiyokuwepo ya mtu fulani au kitu fulani.
-Kuonyesha cheo au kazi anayofanya mtu.
-kuonyesha sifa za mtu.
- kuonyesha umoja wa vitu au watu
-kuonyesha mahali
-kuonyesha umilikishi wa kitu chochote.
                                    6. KIWAKILISHI
Kiwakilishi ni aina ya neno linaloweza kutumika badala ya jina .

            AINA ZA VIWAKILISHI
Viwakilishi vya kuuliza/viwakilishi viulizi ambavyo huashiriwa na mofu / kiambishi {-pi} ambavyo katika tungo hutanguliwa na kiambishi ngeli cha jina husika. Mfano- Mtoto yupi
Wiwakilishi vya urejeshi ambavyo vinajengwa na shina amba pamoja na vipande vidogo vidogo –ye-, -o-, -cho-, vyo, lo, po, mo, ko n.k ambavyo vinachaguliwa kilingana na ngeli ya majina yanayorejeshwa navyo.
Viwakilishi vya idadi: Viwakilishi hivi hutuarifu kuhusu idadi ya nomino hiyo huweza kuwa kamili (halisi) au ya jumla. Mfano; Wengi wamekuja
Viwakilishi vya pekee:-Hivi ni aina ya vivumishi vya pekee kuwakilisha nomino. Hufuata sheria za upatanisho za nomino zinazowakilishwa.
Viwakilishi vya A-unganifu:-Viwakilishi hivi huundwa kwa kihisishi cha A-unganifu kusimamia nominoiliyomilkiwa, inayochukuwa nafasi fulani katika orodha au nomino ya aina fulani.Kihisishi a-unganifu huandamana na nomino kuunda kirai husishi ambacho husimamamahali pa nomino.

                                    7. VIUNGANISHI
Ni maneno, kikundi cha maneno au kiambishi chenye kuunganisha maneno, kirai, kishazi au sentensi.Dhima ya kiunganishi ni kuunga vipashio viwili au zaidi vyenye hadhi sawa kisarufi.

Aina za viunganishi:
·         Viunganishi huru: hivi ni viunganishi vinavyosimama pekee katika tungo, katikati ya vipashio vinavyo ungwa. Hujumuisha: -
-Viunganishi nyongeza/vya kuongeza. Mfano; Tena,Na,Zaidi ya n.k.
- Viunganishi vya sababu/visababishi.  Mfano; Kwa kuwa,kwa sababukwa vile, kutokana na, n.k.
- Viunganishi linganishi/vya kinyume.  Mfano; Ingawa, Japokuwa, Lakini n.k.
- Viunganishi vya wakati.                      Mfano; kasha, baadaye, Halafu, Baada ya n.k.
- Viunganishi vya masharti.                   Mfano; Kama, Ikiwa, Iwapo n.k
- Viunganishi vihusishi                           Mfano; Cha, La, Wa, Za n.k.

·         Viunganishi tegemezi: Ni viambishi ambavyo hutiwa katika kitenzi cha kishazi tegemezi ili kukiunga na kitenzi kikuu cha kishazi huru ambavyo kwa pamoja huunda sentensi changamano au shurtia. Mfano; -ye-, -po-, -ki-, -cho- na -nge-.



8. Vihusishi
Ni maneno ambayo huonyesha uhusiano uliopo baina ya neno moja na jengine.Vihusishi aghlabu huonyesha uhusiano kati ya nomino au kirai nomino na maneno mengine.
Mambo mbalimbali yanayoweza kuonyeshwa na vihusishi
- huonyesha uhusiano wa kiwakati
- huonyesha uhusiano wa mahali
- huonyesha uhusiano wa kulinganisha
- huonyesha uhusiano wa umilikaji
- huonyesha uhusiano wa sababu/kiini
 Aina za vihusishi
-vihusishi vya wakatiMfano; kabla ya, baada ya n.k
-vihusishi vya mahaliMfano; chini ya, juu ya, ndani ya, mbele ya n.k.
- vihusishi vya ulinganishi/ vya kulinganisha Mfano; kuliko, zaidi ya n.k.
-vihusishi vya sababu/ kusudi/nia Mfano; kwa sababu ya, kwa ajili ya n.k.
-vihusishi vya ala (kifaa)-Mfano; kwa
- vihusishi vimilikishi Mfano; cha, za n.k.
-vihusishi vya namna/jinsi/hali Mfano; moto wa kuotea mbali, macho ya mviringo
Matumizi ya ziada ya kihusishi “kwa”
-kihusishi hiki huonyesha mahali au upande
-kihusishi hiki huonyesha sababu au kisababishi cha jambo
-kihusishi hiki huonyesha wakati
-kihusishi hiki huonyesha sehemu Fulani ya kitu kikubwa
-kihusishi hiki hutumika kuonyesha ‘nia ya pamoja na’
-Kihusishi hiki huonyesha jinsi kitendo kilivyotendeka

                                    9. VIHISISHI / VIINGIZI
            Ni maneno ambayo hudokeza hisia za moyoni mwa mzungumzaji baada ya kuwa katika hali ya furaha, huzuni, majonzi, maumivu, kushangaa, majuto n.k. Mara tunapotumia viingizi katika tungo huathiri tungo hiyo kuifanya kuwa na mshangao, hivyo tunaongeza alama ya mshangao mbele ya tungo hiyo. Kwa kuzingatia hisia tunaweza kuwa na aina ya viingizi zifuatazo:-
·         Viingizi vya huzuni – pole! Jamani! Maskini! N.k
·         Viingizi vya mshangao – waow! Lahaula! Eboo! Haiii! Ati!
·         Viingizi vya kuitika – abee! Lamaa! Naam!
·         Viingizi vya kutakia heri – Inshallah!
·         Viingizi vya kiapo – Wallah! Haki ya nani! Kweli kabisa!
 ZOEZI
1.      Tofautisha majina dhahania naya kipekee.
2.      Fafanua matumizi matano ya vitenzi vishirikishi kwa mifano bayana.
3.      Ainisha maneno katika sentensi zifuatazo:-
a.       Mtoto mzuri ameondoka.
b.      Yusuph na Ndonje hawaelewani.
c.       Kwenye kikapu kuna mboga.
d.      Loo! Huna aibu kumuita.
e.       Atakayekuja awe amejiandaa kujibu maswali.
f.       Nimesoma kitabu lakini sijagundua kinahusu nini.
g.      Mkaribishe, aingie.
h.      Nataka nikija nikute tayari.
i.        Ustaarabu umenishinda.
j.        Mwalimu alisema, tuonane kesho.
4.      Tunga sentensi ukionmesha matumizi matano ya kihusishi ‘kwa’.
5.      Kwa kutumia mifano eleza tofauti ya viunganishi na vihusishi.
6.      Eleza kwa mifano bayana aina tatu za vitenzi.
7.      Onesha matumizi matano ya vielezi katika sentensi.
8.      Kivumishi ni nini? Onesha matumizi matano ya vihusishi vya nomino.
9.      Tunga sentensi sita kwa kila aina ya kiunganishi.
10.  Tumia viingizi vifuatavyo kutunga sentensi sahihi:
a.       Taibu
b.      La hasha
c.       Salale
d.      Mashallah
e.       Ebo




3.      SARUFI MUUNDO
Sarufi muundo hujihusisha na kushughulikia mpangilio na mfuatano wa maneno katika tungo ili yaweze kujitosheleza kimaana. Katika sarufi muundo tunaangalia mijengo ya tungo za kiswahiali.

                                    TUNGO
            Tungo ni huwa ni matokeo ya kuviweka pamoja vipashio sahili vya lugha ili kujengana hata kipashio kikubwa kabisa cha lugha. Tungo ina asili yake katika mzizi ‘Tunga’ ukiwa na maana ya kuibua kitu kipya kabisa au kushikamanisha vitu pamoja ili kupata ‘utungo’.
            Tungo hujidhihirisha katika viwango vine ambavyo hutupatia vipashio vya tungo:-
Ø  Kiwango cha neno ambacho hujengwa na mofimu
Ø  Kiwango cha kirai ambacho hujengwa na neno
Ø  Kiwango cha kishazi ambacho hujengwa na kirai
Ø  Kiwango cha sentensi ambacho hujengwa na kirai au kishazi

1.      NENO
Ni silabi au mkusanyiko wa silabi zinazotamkwa na kuandikwa na kuleta maana katika lugha husika. Neno huundwa na mofimu. Ikiwa ni mofimu huru neno huwa neno huru lakini neno likiundwa na mofimu tegemezi neno huwa changamano. Zipo aina nane za maneno katika lugha ya Kiswahili ambazo ni:-
                                i.            Nomino
                              ii.            Kivumishi
                            iii.            Kiwakilishi
                            iv.            Kitenzi
                              v.            Kielezi
                            vi.            Kiunganishi
                          vii.            Kihisishi na
                        viii.            Kihusishi. (rejelea aina za maneno kwa ufafanuzi zaidi)



2.      KIRAI
Ni kipashio cha lugha ambacho huwa na muundo wa neno moja au zaidi lakini huwa hakina muundo wa kiima na kiarifu. Muundo wa kirai huwa ni wa neno moja au zaidi ambayo huwa pamoja katika mpangilio maalumu wenye kuzingatia uhusiano wa maneno hayo na neno kuu ambalo ndio huwa linabeba aina ya kundi hilo la maneno.
            AINA ZA VIRAI
A.    Kirai nomino (KN)
Hili ni kundi la maneno ambalo hutawaliwa na nomino. Kirai nomino huundwa na maneno yafuatayo:-
o   Nomino pekee. Mfano; Asha anapika, Nyangoye anaimba, Nyegera anacheza (N)
o   Nomino mbili au zaidi zinazounganishwa. Mfano; Mhindi na Sagati wanacheza. (N+U+N)
o   Nomino na kivumishi. Mfano; Mtoto mnene amekuja, Mzee mfupi ameondoka. (N+V)
o   Kiwakilishi pekee. Mfano; Yule ameondoka, Wewe umenena, Wale waliokuja. (W)
o   Kiwakilishi na kivumishi. Mfano; Yule mvivu amerudi, Wewe mlemavu njoo. (W+V)
o   Nomino na kitenzi jina. Mfano; Mchezo wa kusisimua, Wimbo wa kupendeza. (N+Ktj)
o   Nomino na kishazi tegemezi kivumishi. Mfano; Mjukuu aliyepotea, Mheshimiwa aliyeondoka. (N+βV)
B.     Kirai kivumishi (KV)
Hiki ni kirai ambacho muundo wake umejikita katika kivumishi na maneno yanayohusiana na kivumishi katika tungo tungo hiyo. Virai hivi kwa kawaida hujibainisha zaidi kimuundo kama sehemu ya virai nomino. Virai hivi huundwa na:-
o   Kivumishi na Kirai nomino. Mfano; Mwenye mali nyingi, Wenye watoto wengi.
o   Kivumishi na kielezi. Mfano; Mzuri sana, Mweupe pee!,Mweusi tii!, Mbaya sana.
o   Kivumishi na kirai kitenzi. Mfano; Mwenye kupiga gitaa, Mwenye kupenda sana.
o   Kivumishi na kirai kiunganishi. Mfano; Nzuri ya kupendeza, Mpungufu wa akili.
C.    Kirai kitenzi (KT)
Ni kirai ambacho kimekitwa katika kitenzi, au katika uhusiano wa kitenzi na neno au mafungu ya mengine ya maneno. Hii ina maana kwamba, neno kuu katika kirai hiki ni kitenzi. Kirai kitenzi kimeundwa na vipashio vifuatavyo:-

o   Kitenzi pekee. Mfano; amekuja, amekula, ameoga. (T)
o   Kitenzi kisaidizi na kitenzi kikuu. Mfano; Alikua anacheza(Ts+T), Alikua anaweza kuimba. (Ts+Ts+T)
o   Kitenzi kishirikishi na shamirisho. Mfano; Ni mtanashati, Ndiye mwizi, Sio mwelewa. (t+sh)
o   Kitenzi, jina na kielezi. Mfano; Nimepika uji asubuhi
D.    Kirai kielezi
Tofauti na aina nyingine ya virai, miundo ya virai vielezi haielekei kukitwa kwenye mahusiano ya lazima baina ya neno kuu (yaani kielezi ) na neno au fungu la maneno linaloandamana nalo. Badala yake miuundo inayohusika hapa ni ya maneno ambayo hufanya kazi pamoja katika Lugha kama misemo, neno au maneno yanayofuata neno lililotangulia yakifafanua zaidi neno hilo. Zaidi kirai kielezi huelezea namna, wakati, mahali na kinachofanya tendo hilo litendeke. Mfano; Mara nyingi, Sana sana, Polepole, Jana asubuhi, Kesho mchana, n.k.
E.     Kirai kihusishi
Ni kirai ambacho muundo wake umekitwa katika mahusiano baina ya vihusishikwa, na, katika,au kwenye na fungu la maneno linaloandamana nacho. Kwa maneno menginekirai hicho ni kile ambacho neno kuu ni kihusishi. Virai vihusishi japokuwa muundo wake hufanana ila hutofautiana kimaana, zipo maana tatuambazo ni:-
a)      Pahala – kwa baba, katika kabati, kwenye lindo
b)      Utumizi – Kwa kisu, Kwa mkono
c)      Uhusika – Na Mjomba, Na Bibi.
Vilvile kirai kihusishi hutumiwa kutekeleza majukumu yafuatayo katika sentensi:-
ü  Kama kivumishi. Mfano; Penseli ya mjomba, Mkoba wa mama, Koti la babu
ü  Kama kielezi. Mfano; Tulisikiliza kwa makini, Tuliimba kwa shangwe, Tulisoma kwa juhudi
ü  Kama kiwakilishi. Mfano; La mjomba limetupwa, Ya shangazi imeuzwa, Wa nne ameondoka



3.      KISHAZI
Ni aina ya tungo ambayo huwa na kitenzi ndani yake, kitenzi hicho kinaweza kikawa kinakamilisha maana au kisiwe kinajikamilisha kimaana. Kitenzi ambacho huwa kinakamilisha maana huwa ni kitenzi kikuu (T), na kile kisichokuwa kinatoa taarifa kamili huwa ni kitenzi kisaidizi (TS). Kwa mujibu huo tunapata aina mbili za kishazi yaani kishazi huru na kishazi tegemezi.
A.    Kishazi huru (K/Hr)
Aina hii ya kishazi huwa na tabia ya kutoa taarifa ambayo huwa ni kamili katika tungo, hubeba kitenzi kikuu au kishirikishi ndani yake. Kishazi hiki huwa hakihitaji maelezo ya ziada ili kukamilisha maana au taarifa kusudiwa na pia huweza kujitegemea kama sentensi kamili na huwa na muundo wa kiima na kiarifu.
Mfano; Mtoto / anacheza mpira
                  K                     A
            Mwanafunzi / anasoma kitabu
                  K                     A
            Mwanaume / anakufahamu
                  K                     A
           Mwanafunzi /. ni mpole
                  K                     A
B. Kishazi tegemezi (K/ Tg)
Aina hii ya kishazi huwa haitoi taarifa iliyokamili badala yake hutegemea kishazi huru ili kukamilisha taarifa iliyokusudiwa na msemaji. Kishazi hiki hutawaliwa na kitenzi kisaidizi. Kishazi tegemezi kwa upekee wake hakiwezi kutoa taarifa iliyokusudiwa. Vishazi tegemezi hushuka hadhi na kuwa na hadhi ya kikundi cha maneno (kirai).
Mfano;      Mtoto unayemjua
                  Mwanafunzi anayesoma
                  Mahali alipoingia
                  Mama alipomchapa
                  Kaka aliporudi
Vishazi hivyo hapo juu havitoi taarifa iliyokamili ila tunapoviweka pamoja na vishazi huru taarifa iliyokusudiwa hukamilika. Tazama hapa chini:-
Mfano;       Mtoto unayemjua ameondoka
                  Mwanafunzi anayesoma atafaulu
                  Mahali alipoingia ni pachafu
                  Mama alipomchapa aliondoka
                  Kaka aliporudi alinifurahisha
Sifa za kishazi tegemezi
                    i.            Hakikamilishi taarifa pasipokuwepo na kishazi huru
Mfano;       Mtoto anayecheza mpira ameumia
                  Mvulana aliyefaulu mtihani amefurahi
                  Mama alipomkaribisha aliingia ndani
                  ii.            Kinaweza kuondolewa katika tungo bila kuathiri taarifa kusudiwa.
Mfano;      mtoto aliyeugua amepona
                  Mtoto amepona
                  Mama uliyemsalimia pale ameondoka jana.
                  Mama ameondoka jana
                iii.            Hutambulishwa na vitambulishi vya urejeshi vinavyopachikwa katika vitenzi.
Mfano; Anayesoma, Alichookota, Uliokatika, Iliyoibiwa, Alipoingia n.k.
                iv.            Vilevile kashazi tegemezi hutambulishwa na viunganishi tegemezi kwamba, ili, ili kwamba, kwa sababu, mzizi wa amba na kiambishi cha masharti.
Mfano;       Mama alisema kwamba motto ameumia
                  Mvulana ambaye ni kaka yangu amerejea nyumbani
                  Akijua atanichapa
            Vishazi tegemezi vipo vya aina mbili kutokana na majukumu yake kimuundo
A.    Kishazi tegemezi kivumishi (bV)
Kishazi tegemezi kivumishi hufanya kazi ya kuvumisha nomino katika tungo.
      Mfano;            Baba anayenijali
                              Mbwa aliyepotea
                              Mwanafunzi aliyefariki
                              Uliyemuona pale
                              Aliyempenda sana

B.     Kishazi tegemezi kielezi (bE)
 Kishazi hiki hufanya kazi ya kueleza tendo katika tungo na hujitokeza kueleza dhima tofauti tofauti kama ifuatavyo:-
ü  Kueleza mahali tendo linapofanyika. Mfano; Alipoingia (mahali dhahiri), Alimochungulia (ndani ya kitu Fulani), Alikoelekea (mahali pasipo dhahiri)
ü  Kueleza wakati wa tendo. Mfano; Tulipotoka, Alipomchapa, Walipomsema n.k.
ü  Kueleza masharti katika tendo. Mfano; Akirudi, Angekuja, Angelimpiga, Angalijua n.k.
ü  Kueleza namna tendo linavyofanyika. Mfano; Alivyoimba, Walivyopendeza, Tulivyomsifu.
ü  Kueleza kasoro katika kukamilisha tendo. Mfano; Ingawa amesoma, Licha ya kufaulu, Japokua amependekezwa.
ü  Kueleza sababu ya kufanyika kwa tendo. Mfano; Kwa sababu alipendeza, Kwa kuwa hujafaulu, Kwa vile umenisomesha.
                             
4.      SENTENSI
Sentensi ni fungu la maneno ambalo huwa na mhusika wa tendo na tendo lenyewe. Sentensi hujengwa na sehemu kuu mbili yaani kiima na kiarifu. Kiima hutawaliwa na mhusika wa tendo yaani nomino hivyo hubeba kirai nomino na upande wa Kiarifu hutawaliwa na taarifa ya tendo hivyo hubeba kirai kitenzi. Sentensi ndio kipashio cha juu kabisa katika darajia ya vipashio vya lugha.
Sehemu za Sentensi.
v  Kiima hukaliwa na kundi nomino ambayo huwa ni mtenda au mtendwa wa jambo linaloelezewa katika sentensi. Hiki hukaa upande wa kushoto mwa kitenzi au mwanzo ni mwa sentensi. Mfano; Mtoto amesoma, Mvulana anapendwa.
Vipashio vya kiima.
o   Nomino pekee. Mfano; Babu amerudi.
o   Nomino  na Nomino. Mfano; Kaka na Dada wameondoka.
o   Nomino na kivumishi. Mfano; Mtoto mzuri amekojoa.
o   Kiwakilishi pekee. Mfano; Yule amevunjika mguu.
Kiwakilishi na Kivumishi. Mfano; Wewe mpole njoo hapa.
o   Kivumishi na Kiwakilishi. Mfano; Mjinga Yule ameondoka.
o   Kitenzi jina. Mfano; Kulima kunafaida nyingi.
o   Nomino na Kishazi tegemezi kivumishi. Mfano; Mtoto aliyeokolewa amerudishwa kwao.
v  Kiarifu hukaliwa na na maneno yanayoarifu tendo linavyofanyika, litakavyofanywa, lilivyofanywa. Hii ndiyo sehemu inayokuwa na umuhimu zaidi katika sentensi maana ndiyo inayotoa taarifa ya sentensi. Huweza kusimama pekee bila kiima maana wakati mwingine huchukua viwakilishi vya kiima yaani viambishi vya nafsi.
Vipashio vya kiarifu
o   Kitenzi kikuu pekee. Mfano; Amekuja.
o   Kitenzi kisaidizi pamoja na kitenzi kikuu. Mfano; Mtoto alikua anacheza.
o   Kitenzi kishirikishi na Shamirisho. Mfano;  Asha ni mpole
o   Kitenzi kikuu na shamirisho. Mfano; Ninasoma kitabu.
o   Kitenzi kikuu na chagizo. Mfano; Anakwenda polepole.
o   Kitenzi kikuu, shamirisho na chagizo. Mfano; Anaendesha gari kwa kasi.
AINA ZA SENTENSI
1.      Sentensi sahili.
Sentensi sahili ni sentensi ambayo muundo wake ni rahisi. Huwa na muundo wa kishazi huru kimoja. Hivyo hubeba kitenzi kikuu kimoja. Kitenzi hicho kinaweza kuambatana na kitenzi kisaidizi ambacho huwa hakina kiambishi cha utegemezi. Sentensi sahili huwa haifungamani na sentensi nyingine, pia kiima chake huwa kimetajwa wazi na huundwa na kitenzi kikuu kimoja au kitenzi kishirikishi au kitenzi kisaidizi na kitenzi kikuu.
Muundo wa sentensi sahili
i.        Muundo wa kitenzi kikuu peke yake. Mfano;  Anakula, Anaimba, Wanacheza.
ii.      Muundo wa kitenzi kisaidizi na kitenzi kikuu.                                                                             Mfano;          Alikwenda kuchunga.                                                                                                             Huwa anakula.                                                                                                                             Alikuwa amekwenda kulinda.
iii.    Muundo wa kirai nomino na kirai kitenzi.                                                                                    Mfano; Juma ameondoka.                                                                                                             Mwajuma amelalamika sana.                                                                                                 Baba yangu amesafiri jana jioni.                                                                                              Mtoto mweupe mzuri amenibadilishia siku yangu.
iv.    Muundo wa virai vitenzi visaidizi.                                                                                                Mfano; Yusuph ni Mwalimu.                                                                                                                    Dani yumo darasani.                                                                                                                Nyegera ana gari zuri.
2.      Sentensi Changamano
Sentensi changamano huwa na muundo wa kishazi tegemezi na kishazi huru. Kishazi tegemezi huwa na hadhi ya kirai kivumishi au kirai kielezi. Huwa hakijikamilishi kimaana hivyo hutegemea kishazi huru ili kukamilisha maana. Hivyo sentensi changamano huchanganya kishazi tegemezi na kishazi huru pammoja.
Muundo wa sentensi changamano.  
i.                    Muundo wenye kishazi tegemezi kivumishi. (βV)
Mfano; Mbwa aliyepigwa jiwe ameumia vibaya.
             Kijana aliyeanguka chini ameumia.
             Mti uliokatwa umeota tena.
ii.                  Muundo wa kishazi tegemezi kielezi. (βE)
Mfano; Kijana alianguka aliposukumwa.
             Babu alifariki alipofikishwa hospitali.
             Binti alifaulu alipokazana kusoma.
3.      Sentensi shurutia
Sentensi shurutia ni aina ya sentensi ambayo ina muundo wa ngeli za masharti. Sentensi changamano huwa na vishazi tegemezi viwili. Viambishi hivyo vya ngeli ni; -ki-, -nge-, -ngali-, na –ngeli- ambavyo hujitokeza katika kitenzi na hujirudia katika vitenzi vyote viwili, havibadilishwi.
Mfano;      Akirudi, atanikuta.
                  Angeondoka, angefika mapema.
                  Angalinisalimu, ningalimwambia yote.
                  Wangeliambia, ningeliondoka.


4.      Sentensi ambatano
Sentensi ambatano huundwa na sentensi mbili au zaidi ambazo huunganishwa na kiunganishi. Sentensi ambatano huwa na miundo ifuatayo:-
i.                    Muundo wa sentensi sahili mbili au zaidi.
Mfano; Mheshimiwa ameruri lakini mzigo haukununuliwa.
            Bunge la katiba limeanza ila sina uhakika kama tutafanikiwa.
            Mtoto amerejea na wazazi wake wamefurahi.
            Yusuph amefanikiwa bila shaka atakuwa na furaha.
ii.                  Muundo wa sentensi sahili na changamano.
Mfano; Mbuzi amenunuliwa na aliyemnunua ni Baba.
            Mtoro ataadhibiwa pia atajulishwa atakapokosea.
            Baba mzazi analima ila shamba analolima si lake.
iii.                Muundo wa sentensi changamano pekee.
Mfano; Mtoto aliyekuja ameondoka na aliyemleta ameshafika kwake.
            Kijana alikasirika alipomuona ila aliyemuona sio mhusika.
            Alifurahi alipofika japokuwa alipoingia hapakumpendeza.
iv.                Muundo wa virai vitenzi visivyo na kiunganishi.
Mfano; Aambiwe, asirudie.
            Arekebishwe, asikosee.
            Mwache, aende.
            Mwombe, aondoke.
Maneno haya huwa na dhana ya kueleza nia ya kufanya jambo Fulani na huwa havibebi viambishi vya njeo pia vikitengwa huwa sentensi zinazojitegemea.
v.                  Muundo wa sentensi shurutia.
Mfano; Akija nitafurahi ila asipokuja nitahuzunika.
            Angelibakia ningelifurahi lakini angelikubali kulala ningelifurahi zaidi.





ZOEZI
1.      Fafanua dhana ya Tungo kisha taja vipashio vinavojenga tungo.
2.      Eleza tofauti ya kirai na kishazi.
3.      Kirai ni kundi la maneno. Thibitisha kwa aina zake huku ukitolea mifano toshelevu.
4.      Kwa mifano eleza maana ya:-
a.       Kishazi
b.      Kishazi huru
c.       Kishazi tegemezi
5.      Thibitisha kuwa kishazi tegemezi hufafanua nomino na kitenzi.
6.      Ainisha vishazi katika tungo zifuatazo:-
a.       Mtoto mwerevevu ameondoka.
b.      Kabla sijamfahamu nilimsumbua sana.
c.       Katika kikapu kilichojaa niliweka nguo chafu.
d.      Asiyestahili amesifiwa.
e.       Bibi aliyeshikwa uchawi ni jirani yetu.
f.       Mama alikua anapika chakula wakati wgeni walipofika.
g.      Akimaliza kusoma atatupeleka disko.
h.      Angelijua, angeliondoka mapema.
i.        Waliingia msikitini walipotaka kuswali.
j.        Vkombe visivyotakatika visitumike.
7.      Thibitisha kuwa kila sentensi ni kishazi ila si kila kishazi ni sentensi.
8.      Fafanua aina nne za sentensi kwa mifano dhahiri.
9.      Eleza kauli kuwa sentensi ambatano ni sentensi pacha zinazofanana au kutofanana.
10.  Bainisha uvumishaji na uelezi wa sentensi changamano kwa mifano.







UCHANGANUZI WA SENTENSI
Tunapoitenga sentensi katika makundi mbalimbali yanayoiunda sentensi hiyo kutoka kundi kubwa hadi dogo kabisa la leksia (neno), hali hiyo ndiyo inayojulikana kama kuchanganua sentensi. Kuchanganua ni kutolea ufafanuzi wa kitu kwa kukielezea kwa mgawanyo wake. Uchanganuzi wa sentensi hupitia hatua zifuatazo:-
                               I.            Kuiainisha sentensi hiyo. Hapa sentensi hutambulishwa kuwa ni aina gani.
                            II.            Kutenga sentensi hiyo katika sehemu zake mbili zinazoiunda, yaani kiima na kiarifu.
                         III.            Kutambulisha makundi ya maneno yanayopatikana katika sehemu hizo.
                         IV.            Kubainisha aina za maneno yanayounda makundi hayo ya maneno.
                            V.            Kuiandika sentensi hiyo kwa kufuatisha aina zake za maneno.
Ipo pia mikabala miwili ya uchanganuzi wa sentensi ambapo yote hufuata hatua zilezile lakini tofauti inayojitokeza ni matumizi ya istilahi za virai upande wa kiarifu.
A)  Mkabala wa kikazi / kimapokeo. Huu hutenga sentensi katika kiima na kiarifu pia hutumia istilahi; Chagizo badala ya Kirai kielezi (KE), Shamirisho badala ya Kirai nomino (KN), na Prediketa badala ya Kirai kitenzi (KT) ila ni katika upande wa kiarifu.
B)  Mkabala wa kimuundo / kisasa. Huu hutenga sentensi katika Kundi nomino na Kundi kitenz na pia hutumia istilahi za kawaida za virai.













NJIA ZA UCHANGANUZI WA SENTENSI
A.    Njia ya matawi / ngowe (mkabala wa kimuundo).
Mfano.

i.                    Mtoto mzuri amenunuliwa zawadi.

S. Sahili.
    
                       

KN                                                                              KT

N                     V                                                         T                                  E


Mtoto              Mzuri                                       amenunuliwa                           zawadi

Mkabala wa kikazi.

S. Sahili.
    
                        K                                 A

                                                            T                      Ch

                    N                     V                                                    E

                                                                                                                       
             Mtoto                   Mzuri            amenunuliwa            zawadi


ii.                  Mwanafunzi aliyefaulu amehama kimyakimya.
Kimuundo
                                                            S. Changamano

                                                KN                                   KT

                        N                                 βV                                                                  

                                                            Ts                    T                                        E
           
Mwanafunzi                              aliyefaulu      amehama                     Kimyakimya
                                                     
                    Kikazi

S. Changamano

                                                K                                      A

                        N                                 βV                   Pr                     Ch

                                                            Ts                    T                                  E
           
Mwanafunzi                               aliyefaulu              amehama                        Kimyakimya








iii.                Mama anapika na Baba anasoma gazeti.
Kimuundo
                                                      S. Ambatano
          
                                          S1                                       S2

                  KN                              KT     U     KN                  KT

              N                                     T                   N                  T                      E
         
  Mama                            anapika           na     Baba                anasoma          gazeti

                  Kikazi
                                                      S. Ambatano
          
                                          S1                                       S2
                              K                     A      U      K                     A

                  N                                 T                N                     T                      Ch

                                                                                                                        E
         
       Mama                             anapika      na    Baba           anasoma            gazeti








B.     Njia ya maelezo.
Kimuundo.
   Mfano; i. Mtoto mfupi anataka chai.
Hii ni sentensi sahili.
Sentensi sahili hii ina Kirai nomino na kirai kitenzi.
Kirai nomino kimeundwa na Nomino na Kivumishi.
Nomino ni ‘Mtoto’.
Kivumishi ni ‘Mzuri’.
Kirai kitenzi kimeundwa na kitenzi kikuu na kirai nomino.
Kitenzi kikuu ni ‘Anataka’.
Kirai nomino hicho kimeundwa na Jina.
Jina hilo ni ‘Chai’.
Kikazi
Hii ni sentensi sahili.
Sentensi hii imeundwa na Kiima na Kiarifu.
Kiima  kina Jina na Kivumishi.
Jina hilo ni ‘Mtoto’.
Kivumishi hicho ni ‘Mzuri’.
Kiarifu kimeundwa na Kitenzi kikuu na Shamirisho.
Kitenzi kikuu ni ‘Anataka’.
Shamirisho ni ‘Chai’.
ii.                  Mama aliyenipenda ameniletea zawadi cha ajabu Mama yangu amechukia.
Kimuundo.
Sentensi hii ni ambatano.
Sentensi hii ina sentensi mbili zinazounganishwa na kiunganishi.
Sentensi ya kwanza ina Kirai nomino na kirai kitenzi.
Kirai nomino kimeunda na Jina na kishazi tegemezi kivumishi.
Jina ni ‘Mama’.
Kishazi tegemezi kivumishi hicho ni kitenzi kisaidizi.
Kitenzi kisaidizi hicho ni ‘Aliyenipenda’.
Kirai kitenzi kimeundwa na kitenzi kikuu na Jina.
Kitenzi kikuu ni ‘Ameniletea’.
Jina ni ‘zawadi’
Kiunganishi ni ‘Cha ajabu’
Sentensi ya pili imeundwa na kirai nomino na kirai kitenzi.
Kirai nomino hicho kimendwa na Jina na kivumishi.
Jina ni ‘Mama’.
Kivumishi ni ‘yangu’.
Kirai kielezi kimeundwa na kitenzi kikuu.
Kitenzi hicho ni ‘amechukia’.
      Kikazi
Sentensi hii ni ambatano.
Sentensi hii ina sentensi mbili zinazounganishwa na kiunganishi.
Sentensi ya kwanza ina Kiima na Kiarifu.
Kiima kimeundwa na Jina na kishazi tegemezi kivumishi.
Jina ni ‘Mama’.
Kishazi tegemezi kivumishi hicho ni kitenzi kisaidizi.
Kitenzi kisaidizi hicho ni ‘Aliyenipenda’.
Kiarifu kimeundwa na kitenzi kikuu na Shamirisho.
Kitenzi kikuu ni ‘Ameniletea’.
Shamirisho ni ‘zawadi’
Kiunganishi ni ‘Cha ajabu’
Sentensi ya pili imeundwa na kiima na Kiarifu.
Kiima kimendwa na Jina na kivumishi.
Jina ni ‘Mama’.
Kivumishi ni ‘yangu’.
Kiarifu kimeunda na Prediketa.
Prediketa hiyo ni ‘amechukia’.




C.    Njia yamshale au Mstari
Mfano.  Mkamwana wake aliyemzalia mwanae watoto amepata matatizo lakini hakwenda kumuona.
            Kimuundo
S                                 Ambatano
S                                  S1 + U +S2
S1                                                 KN + KT
KN                               N + V + βV
N                                  Mkamwana
V                                   Wake
βV                                Ts + V + N
Ts                                 Aliyemzalia
V                                  Mwanae
N                                  Watoto
KT                                T + KN
T                                   Amepata
KN                                N
N                                  Matatizo
U                                  Lakini
S2                                                  KN +KT
KN                                θ
KT                                 Ts + T
TS                                  Hakwenda
T                                    Kumuona







             Kikazi
S                                 Ambatano
S                                  S1 + U +S2
S1                                                K + A
K                                  N + V + βV
N                                  Mkamwana
V                                  Wake
βV                                Ts + V + N
Ts                                 Aliyemzalia
V                                  Mwanae
N                                  Watoto
A                                   Pr + Sh
Pr                                   Amepata
Sh                                N
N                                  Matatizo
U                                  Lakini
S2                                                  K +A
K                                  θ
A                                 Pr
Pr                                 T + Tj
TS                                  Hakwenda
Tj                                    Kumuona









D.    Njia ya visanduku
Mfano; Kijana aliyemleta ameondoka na mtoto haonekani.
      Kimuundo
                                                 S. Ambatano
                   S1
U
                        S2
        KN
         KT

     KN
      KT
N
βV
         T
U
     N
     T
Kijana
aliyemleta
ameondoka
na
mtoto
haonekani
     N
   TS
       T
U
      N
      T


Kikazi
                                                 S. Ambatano
                   S1
U
                        S2
        K
         A

     K
      A
N
βV
         Pr
U
     N
     Pr
Kijana
aliyemleta
ameondoka
na
mtoto
haonekani
    N
      TS
          T
U
      N
       T








Mfano 2. Mwalimu aliyefukuzwa jana shuleni amerudi kwao.
           Kimuundo
                                                                          S. Changamano
                      KN
                          KT
        N
                       βV
              T
           E
Mwalimu
aliyefukuzwa
jana
shuleni
amerudi
kwao
        N
      Ts
 E1
E2
      T
    E


              Kikazi
                                                                          S. Changamano
                      K
                          A
        N
                       βV
              Pr
           Ch
Mwalimu
aliyefukuzwa
jana
shuleni
amerudi
kwao
        N
      Ts
 E1
E2
      T
    E











ZOEZI
1.      ‘Kila sentensi ni tungo ila si kila tungo ni bsentensi’. Thibitisha kwa mifano ya kutosha.
2.      Kwa mifano eleza maana ya istilahi zifuatazo:-
a.       Kiima
b.      Kiarifu
c.       Yambwa
d.      Shamirisho
e.       Chagizo
f.       Sentensi
g.      Sentensi shurutia
3.      Kwa mifano fafanua miundo tofautitofauti ya aina zifuatazo za sentensi.
a.       Sentensi sahili
b.      Sentensi shurutia
c.       Sentensi ambatano
d.      Sentensi changamano
4.      Taja vipashio vya:-
a.       Kiima
b.      Kiarifu
5.      Bainisha mikabala na hatua za kufuatwa katika kuchanganua sentensi.
6.      Changanua sentensi hii kwa kutumia mikabala yote miwili kwa njia ya Ngowe:
-          Mwanafunzi aliyehitimu amefaulu na amewafurahisha wazazi wake.
7.      Changanua sentensi zifuatazo kwa kufuata maelekezo katika mabano.
-          Mtoto amefariki. (Ngowe – Kimuundo)
-          Mtoto amefika ila aliyemleta hafahamiki. (Mshale – Kikazi)
-          Angelijua, angelisoma kwa kuwa hakusoma ameshindwa mtihani. ( Jedwali – kimuundo na kikazi).
-          Mtu akifa anazikwa lakini Ng’ombe akifa anatupwa. ( Maelezo- kimuundo).




                               NGELI ZA NOMINO
    Ni namna ya kuweka majina katika makundi yanayofanana. Majina ya Kiswahili yanaweza kuwekwa katika makundi mbalimbali. Makundi hayo yamegawa na wanaisimu ya Kiswahili kwa kuzingatia maumbo ya alomofu za umoja na uwingi wa majina (kimofolojia) na kwa kuzingatia namna majina yanavyopatana na viambishi awali vya vitenzi (upatanisho wa kisarufi / kisintaksia).
1.      Kimofolojia: Katika kigezo hiki wanaisimu wameyapanga majina kulingana na alomofu za umoja na uwingi za majina hayo. Huu ni mtazamo mkongwe ambao uliofuatwa na wanasarufi wa kimapokeo wakiongozwa na Meinholf, Broomfield na Ashton mnamo miaka ya 1920 – 50. Uchambuzi ulikua kama ifuatavyo:-
1.      M-
2.      WA-
i). Majina ya viumbe vyenye uhai
ispokuwa mimea. Mfano; Mtoto – Watoto, Mzee – Wazee, Mkurya - Wakurya
ii) Majina yanayotokana na vitenzi
vinavyotaja watu. Mfano; Msomi – Wasomi, Mkulima – Wakulima, Mfanyakazi – Wafanyakazi.
3.     M-
4.      MI-
i). Majina ya mimea. Mfano; Mti – Miti, Mwembe, Miembe, Mpera – Mipera.
ii) Majina ya vitu yanayoanza na M- Mfano; Mto – Mito, Msumari – Misumari.
5.      KI-
6.      VI-
i). Majina ya vitu yanayoanza na ki- (umoja) na vi- (wingi). Mfano; Kiti – Viti, Kisu – Visu, Kikapu – Vikapu.
ii). Majina ya viumbe yanayoambishwa na ch- umoja na vy-uwingi. Mfano; Chura – Vyura, Chakula – Vyakula, Chuma – Vyuma.
7.      JI-
8.      MA-
i). Majina yanayoanza na ji- umoja na ma- uwingi. Mfano; Jicho – Macho, Jini – Majini, Jiwe – Mawe, Jina – Majina.
ii). Majina ya mkopo yenye ma- (wingi). Mfano; Bwana – Mabwana, Shati – Mashati.
iii). Majina yenye kueleza dhanna ya wingi japokuwa hayahesabiki. Maji, Majani, Maua, Maini.
9.      N-
i). Majina ambayo huanza na N inayofuatwa na konsonanti, ch-, d-,
g-, j-, z-, na y- katika umoja na wingi. Mfano; Nchi, Ndama, Ngoma, Njaa, Nzi, Nyasi.
ii). Majina yanayoanza na mb-, mv. Mfano; Mbwa, Mvi.
iii). Majina ya mkopo. Mfano; Taa, redio, Kompyuta, Kalamu.
10.  U-
11.  N-
i). Majina yote yanayoanza na U umoja na N-, mb (wingi). Mfano; Ubao – Mbao, Ulimi – Ndimi, Uso – Nyuso.
12.  U-
13.  MA-
i). Majina yote yanayoanza na uumoja na ma- wingi. Mfano; Uasi – Maasi, Uchweo – Machweo, Ugonjwa – Magonjwa.
14.  KU-
i). Majina yanayotokana na vitenzi yanayoanza na ku- (vitenzi-jina). Mfano; kucheza, Kulima, Kuimba, Kupenda.
15.  PA-

i). Huonesha mahali hasa. Mfano; Pale
16.  MU-
i). Huonesha mahali pa ndani. Mfano; Mule
17.  KU
i). Huonesha mahali pa mbali, pakubwa zaidi au popote. Mfano; Kule

UBORA WA KIGEZO CHA KIMOFOLOJIA
                   I.            Uwezekano wa kuzigawa nomino nyingi za Kiswahili ni mkubwa kwa kuwa nyingi zimegawanyika katika maumbo hayo ya umojha na uwingi.
                II.            Ni kigezo muhimu kwani kinajikita zaidi katika nomino na kivumishi chake peke yake hakigusi aina nyingine ya neno tofauti na kigeso cha kisintaksia ambacho hugusa hadi kitenzi.
             III.            Huwasaidia wanasarufi linganishi kuonesha uhusiano wa lugha za vikoa kimoja.

        UPUNGUFU WA KIGEZO HIKI.
                               I.            Kuna viambishi katika ngeli tofauti vinavyofanana. Mfano Kiambishi M- kinajitokeza katika ngeli ya 1 na 3 na MA- inajitokeza katika ngeli ya 8 na 13.
                            II.            Kuna nomino nyingine ambazo hazijidhihirishi katika umoja na uwingi. Mfano ngeli ya 8 na 9.
2.      Kigezo cha sintaksia /upatanisho wa kisarufi:
   Huu ni mtazamo wa kisasa wa uainishaji wa ngeli ambao umeyagawa majina katika makundi kulingana na upatanisho wa kisarufi kat ya jina na viambishi awali vilivyo katika vitenzi. Kwa mujibu wa mtazamo huu, majina yamepangwa katika makundi tisa ambayo ni:-
1.      A -WA
Mfano; Mtoto anacheza / Watoto wanacheza.
            Mzee analima / Wazee wanalima.
             Mwanafunzi anasoma / Wanafunzi wanasoma.
2.      U – I
Mfano; Mkufu umekatika / Mikufu imekatika.
             Mji umevamiwa / Miji imevamiwa.
             Mkaa umemwagika / Mikaa imemwagika.
3.      LI – YA
Mfano; Gogo limevunjika / Magogo yamevunjika.
             Gari limepotea / Magari yamepotea.
              Jiko limewaka / Majiko yamewaka
4.      KI – VI
Mfano;   Kiapo kimekiukwa / Viapo vimekiukwa.
               Kilima kimesawazishwa / Vilima vimesawazishwa.
               Kikongwe kimeuawa / Vikongwe vimeuawa.
5.      I – ZI
Mfano; Ng’ombe imechinjwa / Ng’ombe zimechinjwa.
             Nguo imechanika / Nguo zimechanika.
              Nchi imekosa amani / Nchi zimekosa amani.
6.      U – ZI
Mfano; Ubao umeandikika / Mbao zimeandikika.
             Ukuta umeanguka / Kuta zimeanguka.
             Uzi umetumika / Nyuzi zimetumika.
7.      U – YA
Mfano; Ugonjwa unatisha / Magonjwa yanatisha.
             Uasi umekithiri / Maasi yamekithiri.
8.      KU
Mfano; Kulima kunachosha.
             Kuimba kwake kunafurahisha.
           Kufurahi kwake kumemponya.
9.      PA – MU - KU
Mfano; Hapa pananuka.
             Humu mna nzi.
             Kule kumebomoka.
UBORA WA KIGEZO CHA KISINTAKSIA
n  Unajitosheleza kwa kuwa kila jina inakuwa na upatanishi wake katika kitenzi.
UPUNGUFU WA KIGEZO HIKI
I.                   Kuna viambishi vinavyojirudia. Mfano, U- kimejitokeza katika ngeli ya 2, 6 na 7.
II.                Huyaweka majina yenye maumbo tofauti katika ngeli moja.
III.             Kunaweza kuwa na utata katika upatanisho kwa baadhi ya majina kama “makala”
      Mfano; Makala yamechapishwa.
                  Makala imechapishwa.
Sentensi hizo zote zinatumika ila hatuna wingi wa makala katika Kiswahili.

ZOEZI
1.      Eleza dhana zifuatazo kwa makini:-
a.       Ngeli za majina
b.      Ngeli za majina kimofolojia
c.       Upatanisho wa kisarufi
2.      Yapange majina yafuatayo kwa kigezo cha sarufi mapokeo:- Nazi, Chungwa, Mtu, Mchanga, Ukuta, Ulimi, Uovu, Chapati, Maliwato, Pale, Panga, Kisima, Godoro, Nhi, Mchungwa.
3.      Fafanua faida na hasara za kila mkabalka wa uainishaji wa ngeli za majina.
4.      Onesha mpangilio wa ngeli za majina kisintaksia kisha uoneshe mapungu yake.










                  NJIA ZA UUNZI WA MISAMIATI
            Msamiati ni jumla ya maneno yanayopatikana katika lugha. Uundaji wa maneno mapya ni ujuzi ulioanza tangu awali mwanadamu alipoipata lugha ili kuiwezesha lugha yake kuwa toshelevu na endelevu. Uundaji wa maneno huja mara baada ya kuwepo kwa vitu vipya mwanadamu anavyokutana navyo katika mazingira yake.
            Kwa nini tuunde maneno mapya?
·         Kuwezesha matumizi ya kawaida yanayobadilika kila siku.
·         Kuwezesha kukua kwa taaluma ya utafsiri.
·         Kupata msamiati kubalifu katika muktadha mahsusi.
·         Kukuza utamaduni wa jamii.
·         Kukidhi haja ya kitaaluma / kielimu.
Njia za uundaji wa maneno.
                               I.            Uradidi, katika njia hii neno au silabi huweza kurudiwa rudiwa ili kupata maneno mapya katika lugha. Neno lote linaporudiwa tunapata urudufu kamili, lakini tukirudia sehemu ya neno tunaita urudufu nusu.
Mfano; polepole, harakaharaka, kizunguzungu, kiwiliwili.
                            II.            Kufupisha maneno, ufupisha hutokea pale tunapochukua herufi za mwanzo za maneno hayo. Kuna aina mbili za ufupisho wa maneno:-
a.       Akronimi ni ufupisho wa kuchukua herufi za mwanzoni mwa maneno tu. Mfano; UKIMWI – Upungufu wa Kinga Mwilini.
CHANETA – Chama cha Netiboli Tanzania.
                                                            TUKI – Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili.
b.      Uhulutishaji (blending) ni ufupisho wa kuweka pamoja vijisehemu vya maneno kuunda neno jipya.
Mfano; Msikwao – Mtu asiye na kwao.
            Joto baridi – Jotoridi
            Mnyama mfu – Nyamafu
                         III.            Kufananisha sauti, baadhi ya maneno ya Kiswahili yametokana na uwigaji wa sauti au dhana ya kitu Fulani.
Mfano; Pikipiki – Limetokana na mlio wa chombo hicho.
Kifaru – zana ya kivita, umbo lake linafanana na kifaru    mnyama.
                         IV.            Kuambatanisha maneno, hapa maneno mawili tofauti hushikamanishwa na kuwa neno moja lenye maana tofauti na ile ya kwanza. Mfano; Mwanakwetu, Mcheza kwao, Mwananchi, Mwanachama, Mfamaji, Mpigambizi n.k.
                            V.            Kutohoa maneno, ni mchakato wa kuhamisha maneno kutoka lugha moja kwenda lugha nyingine na kuyatumia jinsi yalivyo huku yakibadilishwa kuwaq na muundo wa maneno ya lugha hiyo. Kiswahili kimetohoa maneno kutoka lugha mbalimbali kama;
a.      kiingereza maneno kama; shati, baiskeli, kompyuta, trekta, waya, redio n.k.
b.      Kiajemi maneno kama; bafta, kodi, darubini, jemedari, rosheni, randa n.k.
c.       Kihindi maneno kama; kanuni, achali, gari, bajia, bima, tumbaku, dobi n.k.
d.      Kiarabu maneno kama; hisani, salama, shukurani, daima, elimu, kauli, fahamu, mahabusu, ila, kulaki n.k.
e.       Kireno maneno kama; meza, mvinyo, seti, korosho, leso, kopa, roda, dama n.k.

ZOEZI
1.      Eleza njia zilizotumika katika kuunda maneno haya ya Kiswahili.
a.       Kiherehere
b.      Mtukwao
c.       Simu ya mkononi
d.      Baiskeli
e.       UKUTA
f.       Mkono wa tembo
g.      Kifaru









                                    WASIFU WA MWANDISHI
Yusuph P Mhindi, alizaliwa miaka 25 iliyopita mjini Mugumu wilayani Serengeti mkoani Mara. Akiwa na miaka saba baada ya kuzaliwa alianza masomo ya elimu ya msingi katika shule ya msingi Mapinduzi iliyoko Mjini Mugumu wilayani Serengeti – Mara.
Alipohitimu elimu ya msingi, alifanikiwa kujiendeleza na Elimu ya sekondari ambapo alisoma Machochwe Shule ya Upili, Bwasi Shule ya Upili na hatimaye safari yake ya Elimu ya Sekondari ilitamatika akiwa Nyansincha Sekondari huko Mara Tanzania.
Hakuishia hapo alijiimarisha zaidi kielimu baada ya kujiunga na Elimu ya Kidato cha tano na sita kwa mchepuo wa sanaa masomo ya Historia, Kiingereza na Kiswahili katika Shule ya Upili Kibara. Na rehema za Mwenyezi Mungu zikizidi kuwa tunu kwake kwani alifaulu pia.
Alijiunga na Chuo Kikuu cha Mt. Augustino kilichopo Jijini Mwanza kwa Shahada ya Sanaa na Elimu, akiwa amejikita katika masomo ya lugha yaani Kiswahili na Kiingereza nakufanikiwa kufanya utafiti juu ya ‘Athari za Kazi za Wazazi kwa Machaguzi ya Kazi kwa Watoto.’  Alihitimu masomo hayo mwaka  2013.
Ameshawahi kuwa mwalimu wa kujitolea katika shule kadhaa zikiwemo Chitengule Sekondari, Kabasa Sekondari, Nyakurunduma Sekondari, Imani Sekondari na kote huko amekuwa akifundisha zaidi somo la Kiswahili na Kiingereza na sasa ameajiliwa kwa muda katika Taasisi ya Elimu Emarx iliyopo mjini Dodoma kama mwalimu wa somo la Kiswahili.
Hii ni chapa yake ya kwanza kama Kitini na anajitayarisha kufanya mapinduzi katika tasnia ya uandishi wa vitabu vya Taaluma na hata vya kijamii pia.
Mungu mbariki Yusuph P Mhindi, ibariki sekta ya Elimu Tanzania, ibariki Tanzania na bara zima la Afrika.


Anapatikana kupitia:
SIMU - +255 765 304 501
BARUA PEPE  – yusuphpius19@gmail.com
UKURAHAMA / FACEBOOK AC – Yusuph Pius Mtz Huru
UKURASA WA UKURAHAMA – Teaching Advancement

TWITTER – YUSUPH PIUS.

Maoni 16 :

MWL JOSEPH LULEY ISINDIKIRO alisema ...

NI MWANZO MZURI SANA. YAKO MAMBO YA KITAALUAM AMBAYO UNAPASWA KUYASOMA PIA KUJIRIDHISHA ZAIDI. MATHALANI. SAUTI /W/ na /y/ HAZINA SIFA YA KUWEKA KATIKA KUNDI LA KONSONANTI MOJA KWA MOJA KAMA ULIVYOFANYA NA MENGINE MADOGO MADOGO.
MUNGU AKUBARIKI KWA UTHUBUTU

Unknown alisema ...

Nimejifunza kitu chema sana

Unknown alisema ...

Nimejifunza mambo nilokwisha ya sahauu asantee

Unknown alisema ...

Ukiacha maana zake naomba kujua tofauti Kati ya irabu na konsonati

Unknown alisema ...

nimejifunza mengi kupetia hili somo

Unknown alisema ...

Kazi nzuri sanaaa

Unknown alisema ...

Kazi nzuri hongeraa

Unknown alisema ...

Iko vizur naomba nileweshe ni kwa jinsi gani fasihi simulizi imeathiriwa na sayansi na tecnologia katika uwasilishwaji wake

Msuva Wislen alisema ...

Kazi nzuri sana

Unknown alisema ...

Mavoo

Unknown alisema ...

Naomba kujua umuhimu wa sarufi

Unknown alisema ...

Hongera kwa kazi nzuri na stadi Bora ya maisha ya uthubutu

Bila jina alisema ...

Shukran Allah adumishe kazi Yako iwe ya mafanikio

Bila jina alisema ...

Tusaidiane kujua sifa za sarufi

Bila jina alisema ...

Hakika sarufi imechambuli vizuri

Bila jina alisema ...

vizuri sna,nmepata maarifa nliyoyasahau.ubarikiwe.