TABIA
ZA VITENZI VYA KISWAHILI
Vitenzi vya
Kiswahili huwa na tabia tofauti tofauti zinazotokana na dhima za mofimu ambazo
hupachikwa katika vitenzi hivyo, hivyo kulingana na dhima za mofimu, vitenzi
vya Kiswahili huwa na tabia zifuatazo:-
I.
Kutambulisha nafsi. Mfano:- Anayesoma
II.
Kutambulisha tendo. Mfano:- Cheza, Lima,
Imba n.k.
III.
Kutambulisha wakati. Mfano:- Ulikuja
IV.
Kutambulisha hali ya uyakinishi na
ukanushi. Mfano:- Anacheka – Hacheki
V.
Kutambulisha kauli mbalimbali za tendo.
Mfano:- cheza-chezwa-chezewa-chezeka n.k.
VI.
Kutambulisha hali ya tendo. Mfano:-Huimba,
Amekula.
VII.
Kuonesha urejeshi wa mtenda, mtendwa na
mtendewa ambao hujidhihirisha katika ngeli ya nomino iliyotajwa kwa kuzingatia
upatanisho wa kisarufi. Urejeshi huo ni wa O-rejeshi. Katika urejeshi huo vitenzi
hubeba viambishi ngeli vya –O- isipokuwa kama nomino ni ya ngeli ya kwanza
umoja ambapo hutumia –e- badala ya –O-.
Mfano:-
NGELI
|
KIAMBISHI
CHA O- REJESHI
|
MFANO
|
A-WA
|
-YE-
na –O-
|
Aliyepiga / Waliokuja
|
U-I
|
-O-
na –YO-
|
Uliokatwa / Iliyokatwa
|
LI-YA
|
-LO-
na –YO-
|
Lililochanika / Yaliyochanika
|
KI-VI
|
-CHO-
na –VYO-
|
Kilichovunjika / Vilivyovunjika
|
I-ZI
|
-YO-
na –ZO-
|
Iliyofungwa / Zilizofungwa
|
U-ZI
|
-O-
na -ZO
|
Uliokatika / Zilizokatika
|
U-YA
|
-O-
na –ZO-
|
Ulionipata / Yaliyonipata
|
KU
|
-KO-
|
Kulikotokea
|
PA-MU-KU
|
PO-MO-KO
|
Pale alipoingia / Mule alimotokea / Kule alikofunga
|
ZOEZI
1. Fafanua
dhana ya sarufi kisha eleza tanzu zinazoijenga.
2. Eleza
umuhimu wa kujifunza sarufi ya Kiswahili.
3. Onesha
tofauti iliyopo kati ya irabu na konsonanti.
4. Eleza
maana ya silabi na uoneshe kwa mifano miundo mitano ya Silabi za Kiswahili.
5. Nini
maana ya mofimu? Fafanua aina zake.
6. Bainisha
dhima za kila mofimu katika maneno yafuatayo:-
a. Anakula
b. Waliokutafuta
c. Tulipokukosa
d. Nikikukumbuka
e. Aliyempigia
f. Hakufika
g. Huimba
h. Mnavyopendana
i.
Amemtukana
j.
Ungelifika
7. Nini
maana ya uambishaji na mnyumbulkiko wa maneno? Onesha jinsi dhana hizo
zinavyochangia kukuza lugha.
8. Eleza
kauli mbalimbali za vitenzi vya lugha ya Kiswahili.
9. Pachika
viambishi ngeli vya O- rejeshi katika vitenzi vifuatavyo ukibainisha umoja na
uwingi:-
a. Chura
amekufa
b. Kitabu
kimechanika
c. Meza
imevunjika
d. Daftari
limechanika
e. Simu
imeita
f. Ameingia
mahali humu
g. Amepitia
pale
h. Imevunjiwa
kule
10.
A.
Neno
Ni
silabi au mkusanyiko wa silabi zinazotamkwa au kuandikwa ambazo huwa na maana
(maana yaweza kuwa ni ya kileksika au kisarufi).
AINA ZA MANENO
1. NOMINO
Ni aina ya neno ambalo
hutaja mtu, kitu, mahali, hali na kitendo. Mfano; Mwajuma, Kalamu, Mwanza,
Udakitari, Kulima n.k.
Aina za nomino:
·
Nomino
za pekee: Nomino za pekee hutaja na kutambulisha nomino
mahsusi
na
za kipekee. Yaani kuwa kitu ni hicho na wala si chengine chochote. Hizi ni
nomino zinazohusisha majina kama vile ya watu, nchi, miji, mito, milima,maziwa
na bahari. Herufi za kwanza za nomono za pekee huwa kubwa hata kamanomino hizi
zinapatikana katikati ya sentensi. Mfano; baba, Asha, Tanzania, Dodoma,
Kilimanjaro, Victoria n.k
·
Nomino
za jamii: Hizi kwa jina jengine huitwa nomino za jumla.
Nomino hizihazibainishi wazi wazi vitu ambavyo habari zake zinatolewa. Kwa
mfano ikiwa nimtu, mahsusi hatambuliwi. Haituambii kama ni Kelvin, Tuafu ama
Zawadi.Ikiwani ziwa halitambuliwi kama ni Michigan , Victoria au Nyasa, yaani
hutaja vitubila kutaja umahsusi wake kama ilivyo katika nomino za pekee. Hizizinapoandikwa
si lazima zianze kwa herufi kubwa isipokuwa zimetumiwamwanzoni mwa sentensi au
zimetumika kama anuani ya kutajia kitu kama vileMkuu wa Sheria. Katika mfano
huu ‘sheria’ kwa kawaida ni nomino ya kawaida,lakini hapa inaanza kwa herufi
kubwa kwani inataja anuwani ya kipekee. Mfano wa nomino za kawaida ni; Mwanafunzi,
Mwalimu, Mnyama, Mtazamaji, Askari n.k
·
Nomino
za kawaida: Kundi hili la nomino hutumia kigezo cha uwezekano
wakuhesabika kuziainisha. Hapa tunatofautisha kati ya nomino zinazowakilisha
vitu vinavyohesabika kwa upande mmoja, na vile visivyohesabika kwa upande mwengine.
Nomino ya vitu vinavyohesabika vitanda, nyumba, vikombe vitabu kadahlika. Zile
zisizohesabika hurejelea vitu ambavyo hutokea kwa wingi na haviwezi kugawika,
kwa mfano maji, mate, makamasi, maziwa, moshi, mafuta. Aghlabu nomino hizo huwa
sawa katika umoja na wingi.
·
Nomino
za kitenzi jina: Hizi ni nomino zinazohusu vitenzi .
Huundwa kwa kuongezwa kiambishi {ku-} cha unominishaji kwenye mzizi wa kitenzi
cha kitendo halisi ili kukifanya kiwe nomino. Mfano; Kulima, Kucheza, Kuimba
n.k
·
Nomino
dhahania: Hizi ni nomino ambazo hurejelea vitu vinavyoweza
kuhusika na mwanaadamu kupitia milango ya hisia kama macho, mapua, masikio
vidole na ulimi- yaani vitu ambavyo haviwezi kushikika, kuonekana, na kuonjeka.
Mfano; Vita, Njaa, Ugonjwa, Shetani, Mungu n.k
2.
Vivumishi
·
Ni maneno
ambayohutoa ufafanuzi au maelezo ya ziada kuhusu jina ili kuitambulisha vyema.
Aina za vivumishi.
·
Vivumishi vya sifa: hutoa
sifa za nomino /kiwakilishi cha nomino. Sifa hizi huweza kuwa nzuri, mbaya au
yoyote ile.Mfano; mzuri, mbaya, mrembo n.k
·
Vivumishi vya idadi:
vinaweza kujitokeza katika aina tatu ndogondogo.Vivumishivya aina hii hutoa taarifa
kuhusu idadi ya nomino ambazo kiwango chakekimetajwa. Mfano; wawili, watano,
wengi, wachache n.k
·
Vivumishi vya kumiliki: Ni
vivumishi vinavyoonesha kuwa kitu fulani kina milikiwa na mtu au kitu chengine.
Mfano;yangu, yake, yako, kwetu n.k
·
Vivumishi Vioneshi:Vivumishi vya
aina hii huonyesha mahali au upande kitu kilipo. Vivumishi vya aina hiihujengwa
na mzizi {h} kwa vitu vilivyopo karibu na mzizi {le} kwa vitu
vilivyo mbali. Mfano; hapa, pale n.k
·
Vivumishi vya kuuliza: Hivi
ni vivumishi ambavyo hufafanua nomino kwa kuuliza habari zake. Hujibu swali“gani?ipi?
ngapi?”
·
Vivumishi vya pekee:Vivumishi
hivi huitwa vya pekee kwa sababu kila kimojawapo huwa na maana maalumu.Pia kila
kimojawapo huchukua upatanisho wake wa kisarufi kulingana na ngeli yanomino
ambayo kinaivumisha. Mizizi vivumishi hivi niote, o-ote, enye, -enyewe,
-ingine, -ingineo. –ote. Huonyesha ujumla wa kitu au vitu-o-oteKivumishi
cha aina hii kina maana ya “kila”, “bila kubagua”– enyeKivumishi cha
aina hii hutumika kuleta dhanna ya umilikishaji nomino Fulani. –enyeweKivumishi
cha aina hii hutumika kuisisitiza nomino fulani.– ingineKivumishi cha
aina hii huonyesha/huonesha ‘tofauti na’ au ‘zaidi ya’ kitu Fulani. –
ingineoKivumishi cha aina hii hutumika kuonesha/kuonyesha ziadi.
·
Vivumishi vya A- unganifu: Vivumishi
vya aina hii huundwa kwa mzizi wa kihusishi a- unganifu. Kihusishi
hikihuandamana na nomino kuunda kirai husishi ambacho huvumisha nomino
iliyotajwaawali. Vivumishi vya aina hii hutumika kuleta dhanna
zifuatazo:--Umilikaji-Nafasi katika orodha. Mfano; wa kwangu,
wa Juma, ya tano ya Sita n.k
4.
Vielezi
Maana ya
vielezi: Vielezi ni maneno yanayofafanua vitenzi, vivumishi
auvielezi vyengine. Huweza kuarifu kitendo kilichotendeka kilitendeka wapi ,
namnagani na hata mara ngapi?
Aina za vielezi
·
Vielezi vya namna au jinsi.Vielezi vya namna hii huonyesha
jinsi au namna kitendo kilivyotendeka. Vielezi vyanamna vipo vya aina kadhaa.
-
Vielezi vya namna halisi.
Hivi ni vielezi
vinavyotumia maneno ambayo kimsingi yana sura ya vielezi moja kwa
moja katika
uainishaji wa aina za maneno.Mfano; kuimba sana
-Vielezi vya
namna mfanano
Hivi ni vieleziambavyo hutumika
kufananisha vitendo na vivumishi au nomino
mbalimbali.
Hujengwa kwa kuongeza kiambishi (ki-) au kiambishi (vi-). Viambishi
hivi
hujulikana kwa
jina la viambishi vya mfanano.Ulifanya vizuri kumsaidia mwanangu.
-Vielezi vya
namna vikariri
Hivi nivieleziambavyo hufafanua vitenzi kwa
kurudiarudia neno moja mara mbili.Mfano; polepole, harakaharaka.
-
Vielezi vya namna hali
Hivi nivieleziambavyo
hufafanua juu ya kitendo kilichotendeka kimetendeka katika
hali gani.
Mfano; kivivu, kibabe, kizembe, kipole n.k
-
Vielezi vya namna ala/kitumizi
Hivi nivielezi
vinavyotaja vitu ambavyo hutumika kutendea kitendo. Mfano; kwa kisu,
kwa kalamu n.k
-
Vielezi vya namna viigizi.
Hivi vinaelezea
zaidi jinsi tendo lilivyofanyika kwa kuigiza au kufuatisha sauti
inayojitokeza
wakati tendo linapofanyika au kutokea. Mfano; alimpiga paaaah!
·
Vielezi vya idadi. Vielezi vya
namna hii huonyesha kuwa kitendo kilitendeka mara fulani au kwa kiasifulani.
Mfano; amempiga mara mbili
·
Vielezi vya mahali..Vielezi vya
namna hii huonyesha mahali ambapo kitendo kinatokea.Huweza kudokezwakwa
viambishi au kwa maneno kamili. Mfano; amekaa jikoni
·
Vielezi vya wakati:Vielezi vya
namna hii huonyesha wakati wa kutendeka kwa kitendo.Huweza kutokeakama maneno
kamili au hodokezwa kwa kiambishi {po.}Mfano; alimkaribisha alipokuja.
5.
VITENZI
Kitenzi ni neno
linaloeleza jambo lililotendwa au lililotendeka. Kitenzi huarifu lililofanyika
au lililofanywa na kiumbe hai chochote kinachoweza kutenda jambo. Kitenzi cha
Kiswahili huundwa na mzizi pamoja na viambishi vyenye uamilifu wa aina tofauti.
AINA ZA
VITENZI
·
Vitenzi
vikuu (T): Vitenzi vikuu ni vile ambavyo hubeba ujumbemuhimu
wa kiarifu cha sentensi. Mfano; Mtoto amekuja.
·
Vitenzi visaidizi: Hivi
hutoa taarifa ya kusaidia vitenzi vikuu. Hutoa taarifa kama vile uwezekano ,
wakati, hali n.k.Vitenzi visaidizi daima hutumika na vitenzi vikuu, ndivyo
vinavyobeba viambishi vya wakati. Mfano; Alikua
anacheza, Huwa namfurahia.
§ Vitenzi visaidizi huweza kupachikwa urejeshi wa nomino na kusaidia kuifafanua nomino hiyo.
Mfano; motto aliyekua
anacheza. Virejeshi hivyo ni kama; -ye-, -yo-, -o-, -lo-, -cho-, -wo- n.k
·
Vitenzi vishirikishi:
Hivi
ni Vitenzi ambavyo hufanya kazi ya kuunga sehemu mbili za sentensi. Havichukui
viambishi vya nafsi, njeo ama hali.Vitenzi vishirikishi ni vya aina mbili,
ambavyo nikitenzi kishirikishi “ni” cha uyakinishi na kitenzi shirikishi“si” cha ukanushi.
Kazi za kitenzi
kishirikishi
-kushirikisha
vipashio vingine katika sentensi
-Kuonesha tabia
fulani iliyopo au isiyokuwepo ya mtu fulani au kitu fulani.
-Kuonyesha cheo
au kazi anayofanya mtu.
-kuonyesha sifa
za mtu.
- kuonyesha
umoja wa vitu au watu
-kuonyesha
mahali
-kuonyesha
umilikishi wa kitu chochote.
6.
KIWAKILISHI
Kiwakilishi ni
aina ya neno linaloweza kutumika badala ya jina .
AINA ZA VIWAKILISHI
Viwakilishi vya kuuliza/viwakilishi viulizi ambavyo huashiriwa na mofu / kiambishi {-pi}
ambavyo katika tungo hutanguliwa na kiambishi ngeli cha jina husika. Mfano-
Mtoto yupi
Wiwakilishi vya urejeshi ambavyo vinajengwa na shina amba pamoja na vipande vidogo
vidogo –ye-, -o-, -cho-, vyo, lo, po, mo, ko n.k ambavyo
vinachaguliwa kilingana na ngeli ya majina yanayorejeshwa navyo.
Viwakilishi vya idadi: Viwakilishi hivi hutuarifu kuhusu idadi ya nomino hiyo huweza kuwa
kamili (halisi) au ya jumla. Mfano; Wengi wamekuja
Viwakilishi vya pekee:-Hivi ni aina ya vivumishi vya pekee kuwakilisha nomino. Hufuata
sheria za upatanisho za nomino zinazowakilishwa.
Viwakilishi vya A-unganifu:-Viwakilishi hivi huundwa kwa kihisishi cha A-unganifu kusimamia
nominoiliyomilkiwa, inayochukuwa nafasi fulani katika orodha au nomino ya aina
fulani.Kihisishi a-unganifu huandamana na nomino kuunda kirai husishi ambacho
husimamamahali pa nomino.
7. VIUNGANISHI
Ni
maneno, kikundi cha maneno au kiambishi chenye kuunganisha maneno, kirai,
kishazi au sentensi.Dhima ya kiunganishi ni kuunga vipashio viwili au zaidi
vyenye hadhi sawa kisarufi.
Aina za
viunganishi:
·
Viunganishi huru: hivi
ni viunganishi vinavyosimama pekee katika tungo, katikati ya vipashio vinavyo
ungwa. Hujumuisha: -
-Viunganishi
nyongeza/vya kuongeza. Mfano; Tena,Na,Zaidi ya n.k.
- Viunganishi
vya sababu/visababishi. Mfano; Kwa kuwa,kwa
sababukwa vile, kutokana na, n.k.
- Viunganishi
linganishi/vya kinyume. Mfano; Ingawa,
Japokuwa, Lakini n.k.
- Viunganishi
vya wakati. Mfano; kasha,
baadaye, Halafu, Baada ya n.k.
- Viunganishi
vya masharti. Mfano; Kama, Ikiwa, Iwapo n.k
- Viunganishi
vihusishi Mfano; Cha, La, Wa, Za n.k.
·
Viunganishi tegemezi: Ni
viambishi ambavyo hutiwa katika kitenzi cha kishazi tegemezi ili kukiunga na
kitenzi kikuu cha kishazi huru ambavyo kwa pamoja huunda sentensi changamano au
shurtia. Mfano; -ye-, -po-, -ki-, -cho- na -nge-.
8. Vihusishi
Ni
maneno ambayo huonyesha uhusiano uliopo baina ya neno moja na jengine.Vihusishi
aghlabu huonyesha uhusiano kati ya nomino au kirai nomino na maneno mengine.
Mambo mbalimbali
yanayoweza kuonyeshwa na vihusishi
- huonyesha
uhusiano wa kiwakati
- huonyesha
uhusiano wa mahali
- huonyesha
uhusiano wa kulinganisha
- huonyesha
uhusiano wa umilikaji
- huonyesha
uhusiano wa sababu/kiini
Aina za vihusishi
-vihusishi
vya wakatiMfano; kabla ya, baada ya
n.k
-vihusishi vya
mahaliMfano; chini ya, juu ya,
ndani ya, mbele ya n.k.
- vihusishi vya
ulinganishi/ vya kulinganisha Mfano; kuliko, zaidi ya n.k.
-vihusishi vya
sababu/ kusudi/nia Mfano; kwa
sababu ya, kwa ajili ya n.k.
-vihusishi vya
ala (kifaa)-Mfano; kwa
-
vihusishi vimilikishi Mfano; cha, za n.k.
-vihusishi vya
namna/jinsi/hali Mfano; moto wa kuotea mbali, macho ya mviringo
Matumizi
ya ziada ya kihusishi “kwa”
-kihusishi
hiki huonyesha mahali au upande
-kihusishi hiki
huonyesha sababu au kisababishi cha jambo
-kihusishi hiki
huonyesha wakati
-kihusishi hiki
huonyesha sehemu Fulani ya kitu kikubwa
-kihusishi hiki hutumika
kuonyesha ‘nia ya pamoja na’
-Kihusishi hiki
huonyesha jinsi kitendo kilivyotendeka
Anapatikana
kupitia:
SIMU
- +255 765 304 501
UKURAHAMA
/ FACEBOOK AC – Yusuph Pius Mtz Huru
UKURASA
WA UKURAHAMA – Teaching Advancement
TWITTER
– YUSUPH PIUS.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni