UCHANGANUZI
WA SENTENSI
Tunapoitenga
sentensi katika makundi mbalimbali yanayoiunda sentensi hiyo kutoka kundi kubwa
hadi dogo kabisa la leksia (neno), hali hiyo ndiyo inayojulikana kama
kuchanganua sentensi. Kuchanganua ni kutolea ufafanuzi wa kitu kwa kukielezea
kwa mgawanyo wake. Uchanganuzi wa sentensi hupitia hatua zifuatazo:-
I.
Kuiainisha sentensi hiyo. Hapa sentensi
hutambulishwa kuwa ni aina gani.
II.
Kutenga sentensi hiyo katika sehemu zake
mbili zinazoiunda, yaani kiima na kiarifu.
III.
Kutambulisha makundi ya maneno
yanayopatikana katika sehemu hizo.
IV.
Kubainisha aina za maneno yanayounda
makundi hayo ya maneno.
V.
Kuiandika sentensi hiyo kwa kufuatisha
aina zake za maneno.
Ipo
pia mikabala miwili ya uchanganuzi wa sentensi ambapo yote hufuata hatua
zilezile lakini tofauti inayojitokeza ni matumizi ya istilahi za virai upande
wa kiarifu.
A) Mkabala
wa kikazi / kimapokeo. Huu hutenga sentensi katika kiima na kiarifu pia
hutumia istilahi; Chagizo badala ya Kirai kielezi (KE), Shamirisho badala ya
Kirai nomino (KN), na Prediketa badala ya Kirai kitenzi (KT) ila ni katika
upande wa kiarifu.
B)
Mkabala
wa kimuundo / kisasa. Huu hutenga sentensi katika Kundi nomino na Kundi
kitenz na pia hutumia istilahi za kawaida za virai.
NJIA
ZA UCHANGANUZI WA SENTENSI
A. Njia ya matawi / ngowe
(mkabala wa kimuundo).
Mfano.
i.
Mtoto mzuri amenunuliwa zawadi.
S. Sahili.
KN KT
N V T E
Mtoto Mzuri amenunuliwa zawadi
Mkabala wa
kikazi.
S. Sahili.
K A
T Ch
N V
E
Mtoto Mzuri
amenunuliwa zawadi
ii.
Mwanafunzi aliyefaulu amehama
kimyakimya.
Kimuundo
S.
Changamano
KN KT
N βV
Ts T E
Mwanafunzi aliyefaulu amehama Kimyakimya
Kikazi
S. Changamano
K A
N βV Pr Ch
Ts T E
Mwanafunzi aliyefaulu amehama Kimyakimya
iii.
Mama anapika na Baba anasoma gazeti.
Kimuundo
S.
Ambatano
S1
S2
KN KT U KN KT
N T N T E
Mama anapika
na Baba anasoma gazeti
Kikazi
S.
Ambatano
S1
S2
K A U K A
N T N T Ch
E
Mama anapika na Baba anasoma gazeti
B.
Njia
ya maelezo.
Kimuundo.
Mfano; i. Mtoto mfupi anataka chai.
Hii ni sentensi sahili.
Sentensi sahili hii ina Kirai nomino na
kirai kitenzi.
Kirai nomino kimeundwa na Nomino na
Kivumishi.
Nomino ni ‘Mtoto’.
Kivumishi ni ‘Mzuri’.
Kirai kitenzi kimeundwa na kitenzi kikuu
na kirai nomino.
Kitenzi kikuu ni ‘Anataka’.
Kirai nomino hicho kimeundwa na Jina.
Jina hilo ni ‘Chai’.
Kikazi
Hii ni sentensi sahili.
Sentensi hii imeundwa na Kiima na
Kiarifu.
Kiima kina Jina na Kivumishi.
Jina hilo ni ‘Mtoto’.
Kivumishi hicho ni ‘Mzuri’.
Kiarifu kimeundwa na Kitenzi kikuu na
Shamirisho.
Kitenzi kikuu ni ‘Anataka’.
Shamirisho ni ‘Chai’.
ii.
Mama aliyenipenda ameniletea zawadi cha
ajabu Mama yangu amechukia.
Kimuundo.
Sentensi
hii ni ambatano.
Sentensi
hii ina sentensi mbili zinazounganishwa na kiunganishi.
Sentensi
ya kwanza ina Kirai nomino na kirai kitenzi.
Kirai
nomino kimeunda na Jina na kishazi tegemezi kivumishi.
Jina
ni ‘Mama’.
Kishazi
tegemezi kivumishi hicho ni kitenzi kisaidizi.
Kitenzi
kisaidizi hicho ni ‘Aliyenipenda’.
Kirai
kitenzi kimeundwa na kitenzi kikuu na Jina.
Kitenzi
kikuu ni ‘Ameniletea’.
Jina
ni ‘zawadi’
Kiunganishi
ni ‘Cha ajabu’
Sentensi
ya pili imeundwa na kirai nomino na kirai kitenzi.
Kirai
nomino hicho kimendwa na Jina na kivumishi.
Jina
ni ‘Mama’.
Kivumishi
ni ‘yangu’.
Kirai
kielezi kimeundwa na kitenzi kikuu.
Kitenzi
hicho ni ‘amechukia’.
Kikazi
Sentensi
hii ni ambatano.
Sentensi
hii ina sentensi mbili zinazounganishwa na kiunganishi.
Sentensi
ya kwanza ina Kiima na Kiarifu.
Kiima
kimeundwa na Jina na kishazi tegemezi kivumishi.
Jina
ni ‘Mama’.
Kishazi
tegemezi kivumishi hicho ni kitenzi kisaidizi.
Kitenzi
kisaidizi hicho ni ‘Aliyenipenda’.
Kiarifu
kimeundwa na kitenzi kikuu na Shamirisho.
Kitenzi
kikuu ni ‘Ameniletea’.
Shamirisho
ni ‘zawadi’
Kiunganishi
ni ‘Cha ajabu’
Sentensi
ya pili imeundwa na kiima na Kiarifu.
Kiima
kimendwa na Jina na kivumishi.
Jina
ni ‘Mama’.
Kivumishi
ni ‘yangu’.
Kiarifu
kimeunda na Prediketa.
Prediketa
hiyo ni ‘amechukia’.
C.
Njia
yamshale au Mstari
Mfano. Mkamwana wake aliyemzalia mwanae watoto
amepata matatizo lakini hakwenda kumuona.
Kimuundo
S Ambatano
S S1 +
U +S2
S1
KN + KT
KN N + V + βV
N Mkamwana
V Wake
βV Ts + V + N
Ts Aliyemzalia
V Mwanae
N Watoto
KT T + KN
T Amepata
KN N
N Matatizo
U Lakini
S2
KN +KT
KN θ
KT Ts + T
TS Hakwenda
T Kumuona
Kikazi
S Ambatano
S S1 +
U +S2
S1
K + A
K N + V + βV
N Mkamwana
V Wake
βV Ts + V + N
Ts Aliyemzalia
V Mwanae
N Watoto
A Pr + Sh
Pr Amepata
Sh N
N Matatizo
U Lakini
S2
K +A
K θ
A Pr
Pr T + Tj
TS Hakwenda
Tj Kumuona
D.
Njia
ya visanduku
Mfano; Kijana aliyemleta ameondoka na mtoto
haonekani.
Kimuundo
S. Ambatano
|
|||||
S1
|
U
|
S2
|
|||
KN
|
KT
|
|
KN
|
KT
|
|
N
|
βV
|
T
|
U
|
N
|
T
|
Kijana
|
aliyemleta
|
ameondoka
|
na
|
mtoto
|
haonekani
|
N
|
TS
|
T
|
U
|
N
|
T
|
Kikazi
S. Ambatano
|
|||||
S1
|
U
|
S2
|
|||
K
|
A
|
|
K
|
A
|
|
N
|
βV
|
Pr
|
U
|
N
|
Pr
|
Kijana
|
aliyemleta
|
ameondoka
|
na
|
mtoto
|
haonekani
|
N
|
TS
|
T
|
U
|
N
|
T
|
Mfano
2. Mwalimu aliyefukuzwa jana shuleni amerudi kwao.
Kimuundo
S. Changamano
|
|||||
KN
|
KT
|
||||
N
|
βV
|
T
|
E
|
||
Mwalimu
|
aliyefukuzwa
|
jana
|
shuleni
|
amerudi
|
kwao
|
N
|
Ts
|
E1
|
E2
|
T
|
E
|
Kikazi
S. Changamano
|
|||||
K
|
A
|
||||
N
|
βV
|
Pr
|
Ch
|
||
Mwalimu
|
aliyefukuzwa
|
jana
|
shuleni
|
amerudi
|
kwao
|
N
|
Ts
|
E1
|
E2
|
T
|
E
|
ZOEZI
1. ‘Kila
sentensi ni tungo ila si kila tungo ni bsentensi’. Thibitisha kwa mifano ya
kutosha.
2. Kwa
mifano eleza maana ya istilahi zifuatazo:-
a. Kiima
b. Kiarifu
c. Yambwa
d. Shamirisho
e. Chagizo
f. Sentensi
g. Sentensi
shurutia
3. Kwa
mifano fafanua miundo tofautitofauti ya aina zifuatazo za sentensi.
a. Sentensi
sahili
b. Sentensi
shurutia
c. Sentensi
ambatano
d. Sentensi
changamano
4. Taja
vipashio vya:-
a. Kiima
b. Kiarifu
5. Bainisha
mikabala na hatua za kufuatwa katika kuchanganua sentensi.
6. Changanua
sentensi hii kwa kutumia mikabala yote miwili kwa njia ya Ngowe:
-
Mwanafunzi aliyehitimu amefaulu na
amewafurahisha wazazi wake.
7. Changanua
sentensi zifuatazo kwa kufuata maelekezo katika mabano.
-
Mtoto amefariki. (Ngowe – Kimuundo)
-
Mtoto amefika ila aliyemleta hafahamiki.
(Mshale – Kikazi)
-
Angelijua, angelisoma kwa kuwa hakusoma
ameshindwa mtihani. ( Jedwali – kimuundo na kikazi).
-
Mtu akifa anazikwa lakini Ng’ombe akifa
anatupwa. ( Maelezo- kimuundo).
NGELI ZA NOMINO
Ni namna ya kuweka majina katika makundi
yanayofanana. Majina ya Kiswahili yanaweza kuwekwa katika makundi mbalimbali.
Makundi hayo yamegawa na wanaisimu ya Kiswahili kwa kuzingatia maumbo ya
alomofu za umoja na uwingi wa majina (kimofolojia) na kwa kuzingatia namna
majina yanavyopatana na viambishi awali vya vitenzi (upatanisho wa kisarufi /
kisintaksia).
1.
Kimofolojia:
Katika
kigezo hiki wanaisimu wameyapanga majina kulingana na alomofu za umoja na
uwingi za majina hayo. Huu ni mtazamo mkongwe ambao uliofuatwa na wanasarufi wa
kimapokeo wakiongozwa na Meinholf, Broomfield na Ashton mnamo miaka ya 1920 –
50. Uchambuzi ulikua kama ifuatavyo:-
1.
M-
2.
WA-
|
i). Majina ya
viumbe vyenye uhai
ispokuwa
mimea. Mfano; Mtoto – Watoto, Mzee – Wazee, Mkurya - Wakurya
ii) Majina yanayotokana na vitenzi
vinavyotaja
watu. Mfano; Msomi – Wasomi, Mkulima – Wakulima, Mfanyakazi – Wafanyakazi.
|
3.
M-
4.
MI-
|
i). Majina ya mimea.
Mfano; Mti – Miti, Mwembe, Miembe, Mpera – Mipera.
ii) Majina ya vitu
yanayoanza na M- Mfano; Mto – Mito,
Msumari – Misumari.
|
5.
KI-
6.
VI-
|
i). Majina ya
vitu yanayoanza na ki- (umoja) na vi- (wingi). Mfano; Kiti – Viti, Kisu – Visu, Kikapu – Vikapu.
ii). Majina ya
viumbe yanayoambishwa na ch- umoja na vy-uwingi. Mfano; Chura – Vyura, Chakula – Vyakula, Chuma – Vyuma.
|
7.
JI-
8.
MA-
|
i).
Majina
yanayoanza na ji- umoja na ma- uwingi. Mfano; Jicho – Macho, Jini
– Majini, Jiwe – Mawe, Jina – Majina.
ii). Majina ya mkopo yenye ma- (wingi). Mfano; Bwana
– Mabwana, Shati – Mashati.
iii). Majina
yenye kueleza dhanna ya wingi japokuwa hayahesabiki. Maji, Majani, Maua,
Maini.
|
9.
N-
|
i). Majina ambayo huanza na N
inayofuatwa na konsonanti, ch-, d-,
g-, j-, z-, na
y- katika umoja na wingi. Mfano; Nchi, Ndama, Ngoma, Njaa, Nzi, Nyasi.
ii). Majina
yanayoanza na mb-, mv. Mfano; Mbwa, Mvi.
iii). Majina
ya mkopo. Mfano; Taa, redio, Kompyuta, Kalamu.
|
10. U-
11. N-
|
i).
Majina
yote yanayoanza na U umoja na N-, mb (wingi). Mfano; Ubao – Mbao, Ulimi
– Ndimi, Uso – Nyuso.
|
12. U-
13. MA-
|
i). Majina
yote yanayoanza na uumoja na ma- wingi. Mfano; Uasi – Maasi, Uchweo – Machweo, Ugonjwa – Magonjwa.
|
14. KU-
|
i). Majina
yanayotokana na vitenzi yanayoanza na ku- (vitenzi-jina). Mfano; kucheza,
Kulima, Kuimba, Kupenda.
|
15. PA-
|
i).
Huonesha mahali hasa. Mfano; Pale
|
16. MU-
|
i).
Huonesha mahali pa ndani. Mfano; Mule
|
17. KU
|
i).
Huonesha mahali pa mbali, pakubwa zaidi au popote. Mfano; Kule
|
UBORA
WA KIGEZO CHA KIMOFOLOJIA
I.
Uwezekano wa kuzigawa nomino nyingi za Kiswahili
ni mkubwa kwa kuwa nyingi zimegawanyika katika maumbo hayo ya umojha na uwingi.
II.
Ni kigezo muhimu kwani kinajikita zaidi
katika nomino na kivumishi chake peke yake hakigusi aina nyingine ya neno
tofauti na kigeso cha kisintaksia ambacho hugusa hadi kitenzi.
III.
Huwasaidia wanasarufi linganishi
kuonesha uhusiano wa lugha za vikoa kimoja.
UPUNGUFU WA KIGEZO HIKI.
I.
Kuna viambishi katika ngeli tofauti
vinavyofanana. Mfano Kiambishi M- kinajitokeza katika ngeli ya 1 na 3 na MA-
inajitokeza katika ngeli ya 8 na 13.
II.
Kuna nomino nyingine ambazo
hazijidhihirishi katika umoja na uwingi. Mfano ngeli ya 8 na 9.
2.
Kigezo cha sintaksia /upatanisho wa
kisarufi:
Huu ni mtazamo wa kisasa wa uainishaji wa
ngeli ambao umeyagawa majina katika makundi kulingana na upatanisho wa kisarufi
kat ya jina na viambishi awali vilivyo katika vitenzi. Kwa mujibu wa mtazamo
huu, majina yamepangwa katika makundi tisa ambayo ni:-
1. A -WA
Mfano;
Mtoto anacheza / Watoto wanacheza.
Mzee analima / Wazee wanalima.
Mwanafunzi anasoma / Wanafunzi wanasoma.
2.
U
– I
Mfano; Mkufu umekatika / Mikufu imekatika.
Mji umevamiwa
/ Miji imevamiwa.
Mkaa umemwagika / Mikaa imemwagika.
3.
LI
– YA
Mfano;
Gogo limevunjika / Magogo yamevunjika.
Gari limepotea / Magari yamepotea.
Jiko limewaka / Majiko yamewaka
4.
KI
– VI
Mfano;
Kiapo kimekiukwa / Viapo vimekiukwa.
Kilima kimesawazishwa / Vilima vimesawazishwa.
Kikongwe kimeuawa / Vikongwe vimeuawa.
5.
I
– ZI
Mfano; Ng’ombe imechinjwa / Ng’ombe zimechinjwa.
Nguo imechanika / Nguo zimechanika.
Nchi imekosa amani / Nchi zimekosa
amani.
6.
U
– ZI
Mfano; Ubao umeandikika / Mbao zimeandikika.
Ukuta umeanguka / Kuta zimeanguka.
Uzi umetumika
/ Nyuzi zimetumika.
7.
U
– YA
Mfano; Ugonjwa unatisha / Magonjwa yanatisha.
Uasi umekithiri / Maasi yamekithiri.
8.
KU
Mfano; Kulima kunachosha.
Kuimba kwake kunafurahisha.
Kufurahi kwake kumemponya.
9.
PA
– MU - KU
Mfano; Hapa pananuka.
Humu mna nzi.
Kule kumebomoka.
UBORA WA KIGEZO CHA
KISINTAKSIA
n Unajitosheleza
kwa kuwa kila jina inakuwa na upatanishi wake katika kitenzi.
UPUNGUFU WA KIGEZO HIKI
I.
Kuna viambishi vinavyojirudia. Mfano, U-
kimejitokeza katika ngeli ya 2, 6 na 7.
II.
Huyaweka majina yenye maumbo tofauti
katika ngeli moja.
III.
Kunaweza kuwa na utata katika upatanisho
kwa baadhi ya majina kama “makala”
Mfano;
Makala yamechapishwa.
Makala imechapishwa.
Sentensi
hizo zote zinatumika ila hatuna wingi wa makala katika Kiswahili.
ZOEZI
1. Eleza
dhana zifuatazo kwa makini:-
a. Ngeli
za majina
b. Ngeli
za majina kimofolojia
c. Upatanisho
wa kisarufi
2. Yapange
majina yafuatayo kwa kigezo cha sarufi mapokeo:- Nazi, Chungwa, Mtu, Mchanga,
Ukuta, Ulimi, Uovu, Chapati, Maliwato, Pale, Panga, Kisima, Godoro, Nhi,
Mchungwa.
3. Fafanua
faida na hasara za kila mkabalka wa uainishaji wa ngeli za majina.
4. Onesha
mpangilio wa ngeli za majina kisintaksia kisha uoneshe mapungu yake.
NJIA ZA UUNZI WA MISAMIATI
Msamiati
ni jumla ya maneno yanayopatikana katika lugha. Uundaji wa maneno mapya ni
ujuzi ulioanza tangu awali mwanadamu alipoipata lugha ili kuiwezesha lugha yake
kuwa toshelevu na endelevu. Uundaji wa maneno huja mara baada ya kuwepo kwa
vitu vipya mwanadamu anavyokutana navyo katika mazingira yake.
Kwa nini tuunde maneno mapya?
·
Kuwezesha matumizi ya kawaida
yanayobadilika kila siku.
·
Kuwezesha kukua kwa taaluma ya utafsiri.
·
Kupata msamiati kubalifu katika muktadha
mahsusi.
·
Kukuza utamaduni wa jamii.
·
Kukidhi haja ya kitaaluma / kielimu.
Njia
za uundaji wa maneno.
I.
Uradidi,
katika njia hii neno au silabi huweza kurudiwa rudiwa ili kupata maneno mapya
katika lugha. Neno lote linaporudiwa tunapata urudufu kamili, lakini tukirudia
sehemu ya neno tunaita urudufu nusu.
Mfano;
polepole, harakaharaka, kizunguzungu, kiwiliwili.
II.
Kufupisha
maneno, ufupisha hutokea pale tunapochukua herufi za mwanzo
za maneno hayo. Kuna aina mbili za ufupisho wa maneno:-
a. Akronimi
ni ufupisho wa kuchukua herufi za mwanzoni mwa maneno tu. Mfano; UKIMWI –
Upungufu wa Kinga Mwilini.
CHANETA
– Chama cha Netiboli Tanzania.
TUKI
– Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili.
b. Uhulutishaji
(blending) ni ufupisho wa kuweka pamoja vijisehemu vya maneno kuunda neno
jipya.
Mfano;
Msikwao – Mtu asiye na kwao.
Joto
baridi – Jotoridi
Mnyama mfu – Nyamafu
III.
Kufananisha
sauti, baadhi ya maneno ya Kiswahili yametokana na
uwigaji wa sauti au dhana ya kitu Fulani.
Mfano;
Pikipiki – Limetokana na mlio wa chombo hicho.
Kifaru
– zana ya kivita, umbo lake linafanana na kifaru mnyama.
IV.
Kuambatanisha
maneno, hapa maneno mawili tofauti hushikamanishwa na kuwa
neno moja lenye maana tofauti na ile ya kwanza. Mfano; Mwanakwetu, Mcheza kwao,
Mwananchi, Mwanachama, Mfamaji, Mpigambizi n.k.
V.
Kutohoa
maneno, ni mchakato wa kuhamisha maneno kutoka lugha moja
kwenda lugha nyingine na kuyatumia jinsi yalivyo huku yakibadilishwa kuwaq na
muundo wa maneno ya lugha hiyo. Kiswahili kimetohoa maneno kutoka lugha
mbalimbali kama;
a.
kiingereza
maneno kama; shati, baiskeli, kompyuta, trekta, waya, redio n.k.
b.
Kiajemi
maneno
kama; bafta, kodi, darubini, jemedari, rosheni, randa n.k.
c.
Kihindi
maneno
kama; kanuni, achali, gari, bajia, bima, tumbaku, dobi n.k.
d.
Kiarabu
maneno
kama; hisani, salama, shukurani, daima, elimu, kauli, fahamu, mahabusu, ila,
kulaki n.k.
e.
Kireno
maneno
kama; meza, mvinyo, seti, korosho, leso, kopa, roda, dama n.k.
ZOEZI
1. Eleza
njia zilizotumika katika kuunda maneno haya ya Kiswahili.
a. Kiherehere
b. Mtukwao
c. Simu
ya mkononi
d. Baiskeli
e. UKUTA
f. Mkono
wa tembo
g. Kifaru
WASIFU WA MWANDISHI
Yusuph P Mhindi, alizaliwa miaka 25 iliyopita mjini
Mugumu wilayani Serengeti mkoani Mara. Akiwa na miaka saba baada ya kuzaliwa
alianza masomo ya elimu ya msingi katika shule ya msingi Mapinduzi iliyoko
Mjini Mugumu wilayani Serengeti – Mara.
Alipohitimu elimu ya msingi, alifanikiwa
kujiendeleza na Elimu ya sekondari ambapo alisoma Machochwe Shule ya Upili,
Bwasi Shule ya Upili na hatimaye safari yake ya Elimu ya Sekondari ilitamatika
akiwa Nyansincha Sekondari huko Mara Tanzania.
Hakuishia hapo alijiimarisha zaidi kielimu baada ya
kujiunga na Elimu ya Kidato cha tano na sita kwa mchepuo wa sanaa masomo ya
Historia, Kiingereza na Kiswahili katika Shule ya Upili Kibara. Na rehema za
Mwenyezi Mungu zikizidi kuwa tunu kwake kwani alifaulu pia.
Alijiunga na Chuo Kikuu cha Mt. Augustino kilichopo
Jijini Mwanza kwa Shahada ya Sanaa na Elimu, akiwa amejikita katika masomo ya
lugha yaani Kiswahili na Kiingereza nakufanikiwa kufanya utafiti juu ya ‘Athari
za Kazi za Wazazi kwa Machaguzi ya Kazi kwa Watoto.’ Alihitimu masomo hayo mwaka 2013.
Ameshawahi kuwa mwalimu wa kujitolea katika shule
kadhaa zikiwemo Chitengule Sekondari, Kabasa Sekondari, Nyakurunduma Sekondari,
Imani Sekondari na kote huko amekuwa akifundisha zaidi somo la Kiswahili na
Kiingereza na sasa ameajiliwa kwa muda katika Taasisi ya Elimu Emarx iliyopo
mjini Dodoma kama mwalimu wa somo la Kiswahili.
Hii ni chapa yake ya kwanza kama Kitini na
anajitayarisha kufanya mapinduzi katika tasnia ya uandishi wa vitabu vya
Taaluma na hata vya kijamii pia.
Mungu mbariki Yusuph P Mhindi, ibariki sekta ya
Elimu Tanzania, ibariki Tanzania na bara zima la Afrika.
Anapatikana
kupitia:
SIMU
- +255 765 304 501
UKURAHAMA
/ FACEBOOK AC – Yusuph Pius Mtz Huru
UKURASA
WA UKURAHAMA – Teaching Advancement
TWITTER
– YUSUPH PIUS.