SARUFI
Sarufi
nimfumo na kanuni za lugha zinazomwezesha mtumiaji wa lugha kuitumia lugha
husika kwa usahihi. Mfumo huo humwezesha mzungumzaji kutunga sentensi zisizo na
kikomo ambazo hukubalika na wazawa wa lugha wanaoifahamu lugha hiyo barabara. Hivyo ni dhahiri kwamba kila lugha ya
mwanadamu huwa na mpangilio na sheria zinazoilinda ili kuifanya kuwa toshelevu
na sanifu, na uzingatiwaji wa kanuni na taratibu hizo kwa mtumiaji humfanya na
kumtambulisha kama mmilisi wa lugha hiyo.
Sheria
za lugha zimegawanyika katika makundi manne yanayojulikana kama matawi ya Sarufi ambayo ni pamoja na;
matamshi, maumbo, muundo na maana.
1. SARUFI
MATAMSHI
Sarufi
matamshi ni tawi la sarufi ambalo limejikita katika kuchunguza sauti na
matamshiyanayotumika katika lugha Fulani na kulinda matumizi sahihi ya matamshi
hayo baina ya watumiaji wa lugha hiyo. Lugha ya Kiswahili kama zilivyokuwa
lugha zote duniani ina matamshi ya aina mbili; Irabu na konsonanti.
A. Irabu
Irabu
ni aina ya vitamkwa ambavyo hutolewa pasi na kuwepo kizuizichochote katika
mkondo hewa utokao mapafuni ukipitia katika chemba ya kinywana chemba ya pua
kwenda nje. Lugha ya Kiswahili inazo Irabu tano ambazo ni; /a/, /e/, /i/, /o/,
na /u/.
B. Konsonanti
Konsonanti
ni aina ya sauti ambazo hutamkwa kwa kuzuia mkondo hewa kutoka mapafuni,
ukipitia chemba ya kinywa na chemba ya pua kwenda nje. Katika lugha ya
Kiswahili zipo jumla ya konsonanti zifuatazo; /b/, /ch/, /d/, /dh/, /f/, /g/,
/gh/, /h/, /j/, /k/, /l/, /m/, /n/, /ny/, /ng’/, /p/, /r/, /s/, /sh/, /t/,
/th/, /v/, /w/, /y/ na /z/.
2.
SARUFI MAUMBO.
Hili
ni tawi la sarufi ambalo hujishughulisha na uchunguzi wa maumbo mbalimbali ya
maneno katika lugha ya Kiswahili. Maumbo hayo ni; silabi, mofimu na neno
lenyewe.
A.
Silabi
Silabi
ni kipashio cha kifonolojia kinachohusu matamshi ambacho kwacho sauti za
Lugha hutamkwa
mara moja kwa pamoja kama fungu moja la sauti. Kuna aina mbili za silabi, yaani
silabi fungenasilabi huru.
Silabi huruni
zile ambazo huishia na irabu.
Kwa
mfano; la, ma, kwa, mba, n.k.
Ilhalisilabi fungeni zile zinazoishia na
konsonanti ambapo katika lugha ya Kiswahili ni nadra kuzipata maana lugha hii
inatumia silabi huru lakini hupatikana katika maneno ya Kiswahili yanayokopwa
kutoka katika lugha nyingine.
Kwa mfano; Alhamisi – a-l-ha-mi-si
Taksi - ta-k-si
Miundo
ya Silabi za Kiswahili
a. Muundo wa irabu peke yake (I) - Yapo
maneno katika lugha ya Kiswahili yanayoundwa na irabu peke yake kama silabi.
Mfano; u+a = Ua, o+a = Oa, a+u = Au, n.k.
b. Muundo wakonsonanti pekee (K) – Kiswahili
hakina maneno mengi yanayoundwa na silabi pekee isipokuwa maneno machache
ambayo huwa ni ya nazali /M/ na /N/ na huwa zinatumika ama mwanzoni au katikati
ya neno. Mfano; m+ke = Mke, m+bwa = Mbwa, n+chi = Nchi n.k
c. Muundo wa konsonanti na irabu (KI) –
Katika muundo huu konsonanti hutangulia irabu. Mfano; b+a = Ba, k+a = Ka n.k.
d.
Muundo
wa konsonanti mbili na irabu (KKI) – Katika muundo
huukonsonanti mbili hutangulia irabu. Mara nyingi konsonanti ya pili huwa ni
kiyeyusho. Mfano; k+w+a = Kwa, m+w+a = Mwa, b+w+a = bwa, n+d+e = Nde, n.k.
e.
Muundo
wa konsonanti tatu na irabu (KKKI) – Muundo wa namna hii
hujitokeza katika maneno machache. Mfano; Bambwa, Tingwa,
Tindwa,
Mbwa,
n.k.
f.
Muundo
wa silabi funge – Huu hujitokeza katika maneno machache
ambayo huwa ya mkopo. Mfano; Il-ha-li = Ilhali, Lab-da
= Labda
B.
Mofimu
Mofimu ni
kipashio kidogo kabisa cha lugha ambacho kina uwezo wa kusitiri maana ya neno
ambalo kwalo limeundwa. AU ni kipashio kidogo kabisa cha lugha chenye maana
kisarufi.
AINA ZA
MOFIMU
Mofimu huru ni
aina ya mofimu ambayo huweza kusimama pekee na kujitosheleza kimaana yaani huwa
na sifa ya neno. Mfano; mama, Baba, Dada, Kaka, Mjomba, Shangazi n.k. Kwa
kuangalia utagundua kuwa mofimu huru haziwezi kugawanyika zaidi na kubeba maana
kisarufi, kwa maana kwamba mofimu ‘baba’ ikigawanywa ba-ba, ‘ba’ hii haina
maana yoyote kisarufi zaidi ya kuwa silabi.
Mofimu tegemezini
aina ya mofimu ambayo huweza kuvunjwavunjwa na kubeba maana kisarufi, mofimu
tegemezi hutegemeana ili kuleta maana kamili ya neno.
Mfano;
neno ‘anakula’ limeundwa na mofimu zifuatazo:- [a-na-kul-a] ambazo kila moja
hubeba dhana Fulani ya kisarufi.
VIAMBISHI
Ni mofimu zinazopachikwa nyuma au
mbele ya mzizi wa neno ili kubadilisha dhana ya neno. Kwa kuwa mofimu hizo
hupachikwa sehemu mbili tofauti, tunapata aina mbili za viambishi kwa mujibu wa
nafasi zake katika nenoyaani; viambishi awaliambavyo hupachikwa mwanzoni
au nyuma ya mzizi wa neno,viambishi katiambavyo hupachikwa katikati ya
neno (Kiswahili hakina viambishi hivi) na viambishi tamatiambavyo hivi
hupachikwa mbele au mwishoni mwa mzizi wa neno.
Mfano:-
VIAMBISHI
AWALI
|
MZIZI
WA NENO
|
VIAMBISHI
TAMATI
|
NENO
JIPYA
|
||
A
|
na
|
chez
|
ew
|
a
|
Anachezewa
|
Wa
|
li
|
chez
|
ean
|
a
|
Walichezeana
|
Tu
|
ta
|
chez
|
e
|
a
|
Tutachezea
|
1. Viambishi awaliHivi
hupachikwa kabla ya mzizi wa neno na huwa ni vya aina tisa:-
i.
Viambisha awali vya nafsi- hivi hudokeza
upatanishi wa nafsi katika kitenzi, zipo
nafsi tatu, nafsi ya kwanza, ya pili, nay a tatu.
NAFSI
|
UMOJA
|
UWINGI
|
Ya Kwanza
|
Ni-
|
Tu-
|
Ya Pili
|
U-
|
M-
|
Ya Tatu
|
A-
|
Wa-
|
M
Mfano:-Ninalima
Tunacheza
ii.
Viambishi awali vya ngeli- hivi
hupatikana mwanzoni mwa nomino au vivumishi ili kudokeza hali ya umoja na
uwingi.
Mfano:-Mtu
(umoja) – Watu (uwingi)
Msafi (umoja) – Wasafi
(uwingi)
iii.
Viambishi awali vya ukanushi - hivi
hudokeza hali ya uhasi wa tendo. Huwakilishwa na mofimu (ha-) na (si-)
Mfano:- Amekula
(uyakinifu) – Hajala (ukanushi), Nakula (uyakinifu) – Sili
(ukanushi)
iv.
Viambishi awali vya Njeo- hivi hudokeza
nyakati mbalimbali ambazo ni wakati uliopita, uliopo na ujao.
NYAKATI
|
MOFIMU
|
Uliopo
|
-Na-
|
Uliopita
|
-li-
|
Ujao
|
-Ta-
|
Mfano:-
Mlituona
Utakuja
v.
Viambishi awali vya hali- hivi hudokeza
hali mbili za nyakati ambazo ni mazoea ambayo huwakilishwa na mofimu {hu} na
timilifu inayowakilishwa na mofimu {me}.
Mfano:-Hucheza
Amelima
vi.
Viambishi awali vya masharti-hivi
hudokeza hali ya masharti au uwezekano katika tendo. Mofimu hizo ni kama –ki-,
nge-, ngali- n.k.
Mfano:-
ukija
Ungekuja
Angalimkuta
vii.
Kiambishi cha urejeshi wa mtenda (kiima)-
mhiki hudokeza urejeshi wa nomino inayotenda katika kitenzi.
Mfano:
- Aliyekuja {-ye-} hudokeza urejeshi wa mtenda.
viii.
Kiambishi kiwakilishi cha mtendwa au
mtendewa (shamirisho) – hivi huwakilisha mtendwa au mtendewa wa jambo.
Mfano;
Nilimpiga,
Uliukata,
Nimeipenda,
Wameniteta.
ix.
Kiambishi awali cha kujirejea
(kujitendea) – hiki huwakilishwa na mofimu (-ji-)
Mfano;
kujipenda
2.
Viambishi
tamati– Hivi hudokeza kauli mbalimbali za vitenzi.
Mfano: - Anacheza –
kutenda
Unachezwa-
Kutendwa
Utachezewa- Kutendewa
Nimemlia- Kutendea
Wamewasomesha- Kutendesha n.k
Mzizi
|
Kiambishi
cha Kauli
|
Kiambishi
tamati maana
|
Neno
jipya
|
Kauli
|
Viambishi vya kauli
|
Chez
|
a
|
Cheza
|
Kutenda
|
-a
|
|
e
|
a
|
Chezea
|
kutendea
|
-e-
|
|
Pig
|
ian
|
a
|
Pigiana
|
Kutendeana
|
-ian-/-ean-
|
iw
|
a
|
Pigiwa
|
Kutendewa
|
-iw-/ew-
|
|
Som
|
esh
|
a
|
Somesha
|
Kutendesha
|
-ish-/esh-
|
eshw
|
a
|
Someshwa
|
Kutendeshwa
|
-ishw-/eshw-
|
|
Lim
|
ik
|
a
|
Limika
|
Kutendeka
|
-ik-/-ek-
|
an
|
a
|
Limana
|
Kutendana
|
-an-
|
|
w
|
a
|
Limwa
|
Kutendwa
|
-w-
|
DHANA YA MZIZI NA SHINA LA KITENZI
Mzizi
wakitenzini sehemu ya neno inayobakia mara baada
ya kuondoa viambishi vyote vya awali na tamati katika neno hilo. Mfano: -
a-na-chez-a {-chez-}, m-ku-lim-a {-lim-}
Mzizi
fungeni ule ambao hauwezi kujikamilisha kimaana yaani
hauwezi kusimama kama neno. Mfano; -lim-, -chez-, -imb- n.k.
Mzizi
huruni
ule ambao huweza kusimama kama neno na ukichanganuliwa zaidi hupoteza maana
yake ya msingi. Mfano; Kinu, Kazi, Arifu, Sali n.k.
Shina
la kitenzini sehemu ya neno ambayo huongezwa
viambishi fuatishi (tamati) au nisehemu ya neno ambayo hubakia baada ya
kuondolewa viambishi tangulizi. Mfano:- chez+a = cheza, lim+a = lima. Sehemu
hii ya neno hutumika kuundia neno jipya.
Shina
sahili – hili ni shina ambalo huundwa na mofimu moja tu
ambayo ni mzizi wa neno hilo, huwa ni mofimu huru, Mfano; Kesho, jana, kitabu,
jarida n.k.
Shina
changamano – shina hili huundwa na mzizi na kiambishi tamati
maana. Mfano; cheka, lala, lia, kula n.k
Shina
ambatani – shina hili huundwa na mofimu mbili ambazo ni
huru. Mfano; mwana + kwenda = mwanakwenda, mbwa + mwitu = mbwamwitu
UAMBISHAJI
NA MNYUMBULIKO WA MANENO
Uambishaji
Uambishaji
ni ule utaratibu wa kuongeza viambishi katika mzizi wa neno,
ili
kulipa neno maana ya ziada. AU ni hali ya kubadilishabadilisha mofimu katika
mzizi wa neno ili kuonesha upatanisho wa kisarufi katika tungo hiyo.
Kiambishi:
Kiambishi
ni sehemu (mofu) ambayo huambikwa kwenye mzizi wa neno ili kulipa neno hilo
maana ya ziada. Tunapopachika viambishi hivyo mwanzoni mwa mzizi wa neno hali
hiyo huitwa ‘uambishaji’. Uambishaji upo wa aina mbili; Unyambuaji au
unyambulishi: Huu ni aina ya uambishaji unaosababisha neno kubadilika
kutoka kategoria moja hadi nyingine. NaMnyambuliko:Ni aina ya
uambishaji ambao huhusisha kurefusha nenona kuliweka katika hali tofauti za
katagoria ileile.
Uambishaji
wa kategoria mbalimbali za maneno.
Uambishaji wa vitenzi –
Uambishaji
wa vitenzi hujitokeza kwa kutegemea dhima tofauti tofauti za mofimu kama vile:-
i.
Viambishi vya nafsi
ii.
Viambishi vya njeo
iii.
Viambishi vya ukanushi
iv.
Viambishi vya urejeshi
v.
Viambishi vya hali
vi.
Na viambishi vya kujitendea
Mfano; mzizi –lim- unaweza kupachikwa
viambishi hivyo na kuweza kubadilika kidhana kama ifuatavyo:-
A-na-lim-a
Hu-lim-a
U-me-lim-a
Ni-na-vyo-lim-a n.k.
Uambishaji wa majina–
Uambishaji wa majina huwa unazingatia upatanisho wa kisarufi kimofolojia ambao
hujikita katika kuangalia alomofu tofauti zinazowakilisha ngeli moja katika umoja
na uwingi wa majina hayo. Kwa mfano:-
UMOJA
|
WINGI
|
ALOMOFU
|
m-tu
|
Wa-tu
|
M/WA
|
m-ti
|
mi-ti
|
M/MI
|
Ki-ti
|
vi-ti
|
KI/VI
|
u-gonjwa
|
Ma-gonjwa
|
U/MA
|
Ø-fisadi
|
Ma-fisadi
|
Ø/MA
|
Ø-kaka
|
Ø-kaka
|
Ø/ Ø
|
Uambishaji wa vielezi–
Vielezi katika lugha ya Kiswahili havitokani na kategoria nyingine ya maneno,
bali ni maneno ya kawaida yanayopatikana katika lugha na si rahisi kupachika
mofimu yoyote katika maneno hayo isipokuwa vielezi vichache ambavyo hupatikana
kwa kupachikwa kiambishi awali cha namna {ki-} katika kivumishi au nomino
mfano: ki-jinga, ki-janja, ki-toto, ki-raia, ki-puuzi n.k.
Unyambulishaji
Ni hali ya
kupachika viambishi tamati katika mzizi wa neno. Mofimu hizo huitwa mofimu
fuatishi.
Unyambulishaji
wa kategoria mbalimbali za maneno ya Kiswahili.
i.
Viwakilishi.
Mfano; Mimi = miye, Sisi = siye, Ambalo, Ambacho, Ambao, Ambaye n.k.
ii.
Majina.
Mfano:
Nyumba+ni = Nyumbani, Shamba+ni = Shambani, n.k.
iii.
Vivumishi.
Mfano:
Safi = Safisha, Refu = Refushan.k.
iv.
Vitenzi.
Mfano: Lima-limika-limishwa-limwa-limiana-limiwa n.k.
Ukitazama kwa
makini utangundua kwamba unyambulishaji mara nyingi hubadilisha neno kutoka
katika kategoria moja na kuipeleka katika kategoria nyingine.
DHIMA ZA
UNYAMBULISHAJI
i.
Kuongeza msamiati wa lugha ya Kiswahili.
ii.
Kuzalisha kauli mbalimbali za vitenzi
vya Kiswahili
iii.
Hupanua maana ya neno.
Anapatikana
kupitia:
SIMU
- +255 765 304 501
UKURAHAMA
/ FACEBOOK AC – Yusuph Pius Mtz Huru
UKURASA
WA UKURAHAMA – Teaching Advancement
TWITTER
– YUSUPH PIUS.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni