9.
VIHISISHI / VIINGIZI
Ni maneno ambayo
hudokeza hisia za moyoni mwa mzungumzaji baada ya kuwa katika hali ya furaha,
huzuni, majonzi, maumivu, kushangaa, majuto n.k. Mara tunapotumia viingizi
katika tungo huathiri tungo hiyo kuifanya kuwa na mshangao, hivyo tunaongeza
alama ya mshangao mbele ya tungo hiyo. Kwa kuzingatia hisia tunaweza kuwa na
aina ya viingizi zifuatazo:-
·
Viingizi vya huzuni – pole! Jamani! Maskini!
N.k
·
Viingizi vya mshangao – waow! Lahaula!
Eboo! Haiii! Ati!
·
Viingizi vya kuitika – abee! Lamaa!
Naam!
·
Viingizi vya kutakia heri – Inshallah!
·
Viingizi vya kiapo – Wallah! Haki ya
nani! Kweli kabisa!
ZOEZI
1. Tofautisha
majina dhahania naya kipekee.
2. Fafanua
matumizi matano ya vitenzi vishirikishi kwa mifano bayana.
3. Ainisha
maneno katika sentensi zifuatazo:-
a.
Mtoto mzuri ameondoka.
b.
Yusuph na Ndonje hawaelewani.
c.
Kwenye kikapu kuna mboga.
d.
Loo! Huna aibu kumuita.
e.
Atakayekuja awe amejiandaa kujibu
maswali.
f.
Nimesoma kitabu lakini sijagundua
kinahusu nini.
g.
Mkaribishe, aingie.
h.
Nataka nikija nikute tayari.
i.
Ustaarabu umenishinda.
j.
Mwalimu alisema, tuonane kesho.
4. Tunga
sentensi ukionmesha matumizi matano ya kihusishi ‘kwa’.
5. Kwa
kutumia mifano eleza tofauti ya viunganishi na vihusishi.
6. Eleza
kwa mifano bayana aina tatu za vitenzi.
7. Onesha
matumizi matano ya vielezi katika sentensi.
8. Kivumishi
ni nini? Onesha matumizi matano ya vihusishi vya nomino.
9. Tunga
sentensi sita kwa kila aina ya kiunganishi.
10. Tumia
viingizi vifuatavyo kutunga sentensi sahihi:
a.
Taibu
b.
La hasha
c.
Salale
d.
Mashallah
e.
Ebo
1.
SARUFI MUUNDO
Sarufi
muundo hujihusisha na kushughulikia mpangilio na mfuatano wa maneno katika
tungo ili yaweze kujitosheleza kimaana. Katika sarufi muundo tunaangalia
mijengo ya tungo za kiswahiali.
TUNGO
Tungo ni huwa ni matokeo ya kuviweka
pamoja vipashio sahili vya lugha ili kujengana hata kipashio kikubwa kabisa cha
lugha. Tungo ina asili yake katika mzizi ‘Tunga’ ukiwa na maana ya kuibua kitu
kipya kabisa au kushikamanisha vitu pamoja ili kupata ‘utungo’.
Tungo hujidhihirisha katika viwango
vine ambavyo hutupatia vipashio vya tungo:-
Ø Kiwango
cha neno ambacho hujengwa na mofimu
Ø Kiwango
cha kirai ambacho hujengwa na neno
Ø Kiwango
cha kishazi ambacho hujengwa na kirai
Ø Kiwango
cha sentensi ambacho hujengwa na kirai au kishazi
1. NENO
Ni
silabi au mkusanyiko wa silabi zinazotamkwa na kuandikwa na kuleta maana katika
lugha husika. Neno huundwa na mofimu. Ikiwa ni mofimu huru neno huwa neno
huru lakini neno likiundwa na mofimu tegemezi neno huwa changamano.
Zipo aina nane za maneno katika lugha ya Kiswahili ambazo ni:-
i.
Nomino
ii.
Kivumishi
iii.
Kiwakilishi
iv.
Kitenzi
v.
Kielezi
vi.
Kiunganishi
vii.
Kihisishi na
viii.
Kihusishi. (rejelea aina za maneno kwa
ufafanuzi zaidi)
1. KIRAI
Ni kipashio cha lugha
ambacho huwa na muundo wa neno moja au zaidi lakini huwa hakina muundo wa kiima
na kiarifu. Muundo wa kirai huwa ni wa neno moja au zaidi ambayo huwa pamoja
katika mpangilio maalumu wenye kuzingatia uhusiano wa maneno hayo na neno kuu
ambalo ndio huwa linabeba aina ya kundi hilo la maneno.
AINA ZA VIRAI
A. Kirai nomino (KN)
Hili ni kundi la
maneno ambalo hutawaliwa na nomino. Kirai nomino huundwa na maneno yafuatayo:-
o
Nomino pekee. Mfano; Asha
anapika, Nyangoye anaimba, Nyegera anacheza (N)
o
Nomino mbili au zaidi zinazounganishwa.
Mfano; Mhindi na Sagati wanacheza. (N+U+N)
o
Nomino na kivumishi. Mfano; Mtoto
mnene amekuja, Mzee mfupi ameondoka. (N+V)
o
Kiwakilishi pekee. Mfano; Yule
ameondoka, Wewe umenena, Wale waliokuja. (W)
o
Kiwakilishi na kivumishi. Mfano; Yule
mvivu amerudi, Wewe mlemavu njoo. (W+V)
o
Nomino na kitenzi jina. Mfano; Mchezo
wa kusisimua, Wimbo wa kupendeza. (N+Ktj)
o
Nomino na kishazi tegemezi kivumishi.
Mfano; Mjukuu aliyepotea, Mheshimiwa aliyeondoka. (N+βV)
B. Kirai kivumishi (KV)
Hiki
ni kirai ambacho muundo wake umejikita katika kivumishi na maneno yanayohusiana
na kivumishi katika tungo tungo hiyo. Virai hivi kwa kawaida hujibainisha zaidi
kimuundo kama sehemu ya virai nomino. Virai hivi huundwa na:-
o
Kivumishi na Kirai nomino. Mfano; Mwenye
mali nyingi, Wenye watoto wengi.
o
Kivumishi na kielezi. Mfano; Mzuri sana,
Mweupe
pee!,Mweusi tii!, Mbaya sana.
o
Kivumishi na kirai kitenzi. Mfano; Mwenye
kupiga gitaa, Mwenye kupenda sana.
o
Kivumishi na kirai kiunganishi. Mfano; Nzuri
ya kupendeza, Mpungufu wa akili.
C. Kirai kitenzi (KT)
Ni
kirai ambacho kimekitwa katika kitenzi, au katika uhusiano wa kitenzi na neno
au mafungu ya mengine ya maneno. Hii ina maana kwamba, neno kuu katika kirai
hiki ni kitenzi. Kirai kitenzi kimeundwa na vipashio vifuatavyo:-
o
Kitenzi pekee. Mfano; amekuja,
amekula,
ameoga.
(T)
o
Kitenzi kisaidizi na kitenzi kikuu.
Mfano; Alikua anacheza(Ts+T), Alikua anaweza kuimba. (Ts+Ts+T)
o
Kitenzi kishirikishi na shamirisho.
Mfano; Ni mtanashati, Ndiye mwizi, Sio mwelewa. (t+sh)
o
Kitenzi, jina na kielezi. Mfano; Nimepika
uji asubuhi
D. Kirai kielezi
Tofauti
na aina nyingine ya virai, miundo ya virai vielezi haielekei kukitwa kwenye
mahusiano ya lazima baina ya neno kuu (yaani kielezi ) na neno au fungu la
maneno linaloandamana nalo. Badala yake miuundo inayohusika hapa ni ya maneno
ambayo hufanya kazi pamoja katika Lugha kama misemo, neno au maneno yanayofuata
neno lililotangulia yakifafanua zaidi neno hilo. Zaidi kirai kielezi huelezea
namna, wakati, mahali na kinachofanya tendo hilo litendeke. Mfano; Mara nyingi,
Sana sana, Polepole, Jana asubuhi, Kesho mchana, n.k.
E. Kirai kihusishi
Ni
kirai ambacho muundo wake umekitwa katika mahusiano baina ya vihusishikwa, na,
katika,au kwenye na fungu la maneno linaloandamana nacho. Kwa maneno
menginekirai hicho ni kile ambacho neno kuu ni kihusishi. Virai vihusishi
japokuwa muundo wake hufanana ila hutofautiana kimaana, zipo maana tatuambazo
ni:-
a)
Pahala – kwa baba, katika kabati, kwenye
lindo
b)
Utumizi – Kwa kisu, Kwa mkono
Vilvile
kirai kihusishi hutumiwa kutekeleza majukumu yafuatayo katika sentensi:-
ü Kama
kivumishi. Mfano; Penseli ya mjomba, Mkoba
wa mama, Koti la babu
ü Kama
kielezi. Mfano; Tulisikiliza kwa makini,
Tuliimba kwa shangwe, Tulisoma kwa juhudi
ü Kama
kiwakilishi. Mfano; La mjomba
limetupwa, Ya shangazi imeuzwa, Wa nne ameondoka
2. KISHAZI
Ni
aina ya tungo ambayo huwa na kitenzi ndani yake, kitenzi hicho kinaweza kikawa
kinakamilisha maana au kisiwe kinajikamilisha kimaana. Kitenzi ambacho huwa
kinakamilisha maana huwa ni kitenzi kikuu (T), na kile kisichokuwa kinatoa
taarifa kamili huwa ni kitenzi kisaidizi (TS). Kwa mujibu huo tunapata aina
mbili za kishazi yaani kishazi huru
na kishazi tegemezi.
A.
Kishazi
huru (K/Hr)
Aina
hii ya kishazi huwa na tabia ya kutoa taarifa ambayo huwa ni kamili katika
tungo, hubeba kitenzi kikuu au kishirikishi ndani yake. Kishazi hiki huwa
hakihitaji maelezo ya ziada ili kukamilisha maana au taarifa kusudiwa na pia
huweza kujitegemea kama sentensi kamili na huwa na muundo wa kiima na kiarifu.
Mfano;
Mtoto / anacheza mpira
K A
Mwanafunzi / anasoma kitabu
K A
Mwanaume / anakufahamu
K A
Mwanafunzi /. ni mpole
K A
B. Kishazi tegemezi (K/ Tg)
Aina
hii ya kishazi huwa haitoi taarifa iliyokamili badala yake hutegemea kishazi
huru ili kukamilisha taarifa iliyokusudiwa na msemaji. Kishazi hiki hutawaliwa
na kitenzi kisaidizi. Kishazi tegemezi kwa upekee wake hakiwezi kutoa taarifa
iliyokusudiwa. Vishazi tegemezi hushuka hadhi na kuwa na hadhi ya kikundi cha
maneno (kirai).
Mfano; Mtoto unayemjua
Mwanafunzi anayesoma
Mahali alipoingia
Mama alipomchapa
Kaka aliporudi
Vishazi
hivyo hapo juu havitoi taarifa iliyokamili ila tunapoviweka pamoja na vishazi
huru taarifa iliyokusudiwa hukamilika. Tazama hapa chini:-
Mfano; Mtoto
unayemjua ameondoka
Mwanafunzi anayesoma atafaulu
Mahali alipoingia ni pachafu
Mama alipomchapa aliondoka
Kaka aliporudi alinifurahisha
Sifa za kishazi tegemezi
i.
Hakikamilishi taarifa pasipokuwepo na
kishazi huru
Mfano; Mtoto
anayecheza mpira ameumia
Mvulana aliyefaulu mtihani amefurahi
Mama
alipomkaribisha aliingia ndani
ii.
Kinaweza kuondolewa katika tungo bila
kuathiri taarifa kusudiwa.
Mfano; mtoto aliyeugua
amepona
Mtoto amepona
Mama uliyemsalimia pale ameondoka jana.
Mama ameondoka jana
iii.
Hutambulishwa na vitambulishi vya
urejeshi vinavyopachikwa katika vitenzi.
Mfano;
Anayesoma, Alichookota, Uliokatika, Iliyoibiwa, Alipoingia
n.k.
iv.
Vilevile kashazi tegemezi hutambulishwa
na viunganishi tegemezi kwamba, ili, ili kwamba, kwa sababu, mzizi wa amba na
kiambishi cha masharti.
Mfano; Mama
alisema kwamba motto ameumia
Mvulana ambaye ni kaka yangu amerejea nyumbani
Akijua
atanichapa
Vishazi tegemezi vipo vya aina mbili
kutokana na majukumu yake kimuundo
A.
Kishazi tegemezi
kivumishi (bV)
Kishazi tegemezi kivumishi hufanya kazi
ya kuvumisha nomino katika tungo.
Mfano;
Baba anayenijali
Mbwa
aliyepotea
Mwanafunzi
aliyefariki
Uliyemuona pale
Aliyempenda sana
B.
Kishazi
tegemezi kielezi (bE)
Kishazi hiki hufanya kazi ya kueleza tendo
katika tungo na hujitokeza kueleza dhima tofauti tofauti kama ifuatavyo:-
ü Kueleza
mahali tendo linapofanyika. Mfano; Alipoingia
(mahali dhahiri), Alimochungulia (ndani ya kitu Fulani),
Alikoelekea
(mahali pasipo dhahiri)
ü Kueleza
wakati wa tendo. Mfano; Tulipotoka,
Alipomchapa,
Walipomsema
n.k.
ü Kueleza masharti katika tendo. Mfano; Akirudi,
Angekuja,
Angelimpiga,
Angalijua
n.k.
ü Kueleza
namna tendo linavyofanyika. Mfano;
Alivyoimba,
Walivyopendeza,
Tulivyomsifu.
ü Kueleza
kasoro katika kukamilisha tendo.
Mfano; Ingawa amesoma, Licha ya kufaulu, Japokua
amependekezwa.
ü Kueleza
sababu ya kufanyika kwa tendo. Mfano;
Kwa
sababu alipendeza, Kwa kuwa hujafaulu, Kwa
vile umenisomesha.
3. SENTENSI
Sentensi
ni fungu la maneno ambalo huwa na mhusika wa tendo na tendo lenyewe. Sentensi
hujengwa na sehemu kuu mbili yaani kiima na kiarifu. Kiima hutawaliwa na
mhusika wa tendo yaani nomino hivyo hubeba kirai nomino na upande wa Kiarifu
hutawaliwa na taarifa ya tendo hivyo hubeba kirai kitenzi. Sentensi ndio
kipashio cha juu kabisa katika darajia ya vipashio vya lugha.
Sehemu
za Sentensi.
v Kiima
hukaliwa na kundi nomino ambayo huwa ni mtenda au mtendwa wa jambo
linaloelezewa katika sentensi. Hiki hukaa upande wa kushoto mwa kitenzi au
mwanzo ni mwa sentensi. Mfano; Mtoto amesoma,
Mvulana
anapendwa.
Vipashio vya kiima.
o
Nomino pekee. Mfano; Babu amerudi.
o
Nomino
na Nomino. Mfano; Kaka na Dada
wameondoka.
o
Nomino na kivumishi. Mfano; Mtoto mzuri amekojoa.
o
Kiwakilishi pekee. Mfano; Yule amevunjika mguu.
Kiwakilishi na Kivumishi. Mfano; Wewe mpole njoo hapa.
o
Kivumishi na Kiwakilishi. Mfano; Mjinga Yule ameondoka.
o
Kitenzi jina. Mfano; Kulima kunafaida nyingi.
o
Nomino na Kishazi tegemezi kivumishi.
Mfano; Mtoto aliyeokolewa
amerudishwa kwao.
v Kiarifu hukaliwa
na na maneno yanayoarifu tendo linavyofanyika, litakavyofanywa, lilivyofanywa.
Hii ndiyo sehemu inayokuwa na umuhimu zaidi katika sentensi maana ndiyo
inayotoa taarifa ya sentensi. Huweza kusimama pekee bila kiima maana wakati
mwingine huchukua viwakilishi vya kiima yaani viambishi vya nafsi.
Vipashio
vya kiarifu
o
Kitenzi kikuu pekee. Mfano; Amekuja.
o
Kitenzi kisaidizi pamoja na kitenzi
kikuu. Mfano; Mtoto alikua anacheza.
o
Kitenzi kishirikishi na Shamirisho.
Mfano; Asha ni mpole
o
Kitenzi kikuu na shamirisho. Mfano; Ninasoma kitabu.
o
Kitenzi kikuu na chagizo. Mfano; Anakwenda polepole.
o
Kitenzi kikuu, shamirisho na chagizo.
Mfano; Anaendesha gari kwa kasi.
AINA ZA SENTENSI
1.
Sentensi
sahili.
Sentensi sahili ni sentensi ambayo muundo wake ni rahisi.
Huwa na muundo wa kishazi huru kimoja. Hivyo hubeba kitenzi kikuu kimoja.
Kitenzi hicho kinaweza kuambatana na kitenzi kisaidizi ambacho huwa hakina
kiambishi cha utegemezi. Sentensi sahili huwa haifungamani na sentensi
nyingine, pia kiima chake huwa kimetajwa wazi na huundwa na kitenzi kikuu
kimoja au kitenzi kishirikishi au kitenzi kisaidizi na kitenzi kikuu.
Muundo wa
sentensi sahili
i.
Muundo wa kitenzi kikuu peke yake. Mfano; Anakula, Anaimba, Wanacheza.
ii. Muundo wa
kitenzi kisaidizi na kitenzi kikuu. Mfano; Alikwenda
kuchunga. Huwa anakula. Alikuwa
amekwenda kulinda.
iii. Muundo wa kirai
nomino na kirai kitenzi. Mfano;
Juma ameondoka. Mwajuma
amelalamika sana. Baba
yangu amesafiri jana jioni. Mtoto
mweupe mzuri amenibadilishia siku yangu.
iv. Muundo wa
virai vitenzi visaidizi. Mfano;
Yusuph ni Mwalimu. Dani
yumo darasani. Nyegera
ana gari zuri.
2.
Sentensi
Changamano
Sentensi changamano
huwa na muundo wa kishazi tegemezi na kishazi huru. Kishazi tegemezi huwa na
hadhi ya kirai kivumishi au kirai kielezi. Huwa hakijikamilishi kimaana hivyo
hutegemea kishazi huru ili kukamilisha maana. Hivyo sentensi changamano
huchanganya kishazi tegemezi na kishazi huru pammoja.
Muundo
wa sentensi changamano.
i.
Muundo wenye kishazi tegemezi kivumishi.
(βV)
Mfano;
Mbwa aliyepigwa jiwe ameumia vibaya.
Kijana aliyeanguka
chini ameumia.
Mti uliokatwa umeota tena.
ii.
Muundo wa kishazi tegemezi kielezi. (βE)
Mfano;
Kijana alianguka aliposukumwa.
Babu alifariki alipofikishwa
hospitali.
Binti alifaulu alipokazana
kusoma.
3.
Sentensi
shurutia
Sentensi
shurutia ni aina ya sentensi ambayo ina muundo wa ngeli za masharti. Sentensi
changamano huwa na vishazi tegemezi viwili. Viambishi hivyo vya ngeli ni; -ki-,
-nge-, -ngali-, na –ngeli- ambavyo hujitokeza katika kitenzi na hujirudia
katika vitenzi vyote viwili, havibadilishwi.
Mfano; Akirudi,
atanikuta.
Angeondoka, angefika
mapema.
Angalinisalimu, ningalimwambia
yote.
Wangeliambia, ningeliondoka.
4.
Sentensi
ambatano
Sentensi
ambatano huundwa na sentensi mbili au zaidi ambazo huunganishwa na kiunganishi.
Sentensi ambatano huwa na miundo ifuatayo:-
i.
Muundo wa sentensi sahili mbili au
zaidi.
Mfano;
Mheshimiwa ameruri lakini mzigo haukununuliwa.
Bunge la katiba limeanza ila sina
uhakika kama tutafanikiwa.
Mtoto amerejea na wazazi wake
wamefurahi.
Yusuph amefanikiwa bila shaka
atakuwa na furaha.
ii.
Muundo wa sentensi sahili na changamano.
Mfano; Mbuzi amenunuliwa na aliyemnunua
ni Baba.
Mtoro
ataadhibiwa pia atajulishwa atakapokosea.
Baba
mzazi analima ila shamba analolima si lake.
iii.
Muundo wa sentensi changamano pekee.
Mfano;
Mtoto aliyekuja ameondoka na aliyemleta ameshafika kwake.
Kijana alikasirika alipomuona ila
aliyemuona sio mhusika.
Alifurahi alipofika japokuwa
alipoingia hapakumpendeza.
iv.
Muundo wa virai vitenzi visivyo na kiunganishi.
Mfano;
Aambiwe, asirudie.
Arekebishwe, asikosee.
Mwache, aende.
Mwombe, aondoke.
Maneno
haya huwa na dhana ya kueleza nia ya kufanya jambo Fulani na huwa havibebi
viambishi vya njeo pia vikitengwa huwa sentensi zinazojitegemea.
v.
Muundo wa sentensi shurutia.
Mfano;
Akija nitafurahi ila asipokuja nitahuzunika.
Angelibakia ningelifurahi lakini
angelikubali kulala ningelifurahi zaidi.
ZOEZI
1. Fafanua
dhana ya Tungo kisha taja vipashio vinavojenga tungo.
2. Eleza
tofauti ya kirai na kishazi.
3. Kirai
ni kundi la maneno. Thibitisha kwa aina zake huku ukitolea mifano toshelevu.
4. Kwa
mifano eleza maana ya:-
a.
Kishazi
b.
Kishazi huru
c.
Kishazi tegemezi
5. Thibitisha
kuwa kishazi tegemezi hufafanua nomino na kitenzi.
6. Ainisha
vishazi katika tungo zifuatazo:-
a.
Mtoto mwerevevu ameondoka.
b.
Kabla sijamfahamu nilimsumbua sana.
c.
Katika kikapu kilichojaa niliweka nguo
chafu.
d.
Asiyestahili amesifiwa.
e.
Bibi aliyeshikwa uchawi ni jirani yetu.
f.
Mama alikua anapika chakula wakati wgeni
walipofika.
g.
Akimaliza kusoma atatupeleka disko.
h.
Angelijua, angeliondoka mapema.
i.
Waliingia msikitini walipotaka kuswali.
j.
Vkombe visivyotakatika visitumike.
7. Thibitisha
kuwa kila sentensi ni kishazi ila si kila kishazi ni sentensi.
8. Fafanua
aina nne za sentensi kwa mifano dhahiri.
9. Eleza
kauli kuwa sentensi ambatano ni sentensi pacha zinazofanana au kutofanana.
10. Bainisha
uvumishaji na uelezi wa sentensi changamano kwa mifano.
Anapatikana
kupitia:
SIMU
- +255 765 304 501
UKURAHAMA
/ FACEBOOK AC – Yusuph Pius Mtz Huru
UKURASA
WA UKURAHAMA – Teaching Advancement
TWITTER
– YUSUPH PIUS.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni